November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TPDC kuunganisha na gesi asilia nyumba 1000

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MENEJA Biashara wa Gesi Asilia kutoka Shirika la Maendeeo ya Petroli (TPDC) Mhandisi Emmanuel Gilbert amesema Shirika hilo limekuwa ni moja ya watu wanaounga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha nchi inakuwa na matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumza na waandisgi wa habari kwenye maonesho ya wiki ya Nishati 2024 Bungeni jijini Dodoma,Mhandidi Gibert amesema Shirika hilo linaunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia kwenye kuunganisha matumizi ya gesi asilia majumbani .

“Kwa hiyo ni sehemu ya mchango mkubwa wa kufikia lengo la asilimia 85 ya kaya zote hapa nchini ziwe zinatumia Nishati safi ya kupikia itakapofika 2030, na hii ndiyo sera ya nishati safi ya kupikia.”amesema Mhandisi Gibert
Aidha amesema TPDC pia inatekeleza miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa kuunganisha gesi asilia kwenye nyumba 1000 ambapo hadi kufika mei mwaka huu watakuwa wameshapata mkandarasi ambapo nyumba 500 zitakuwa Mnazi Mmoja mkoani Lindi na nyingine 500 zitakuwa Mkuranga mkoani Pwani.

“Kwa hiyo kwa makadirio tuliyonayo hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei mkandarasi atakuwa saiti kwenye maeneo hayo mawili kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uunganishanishaji wa miundombinu kwenye hizo nyumba 1000.”amesema  

Hata hivyo amesema tayari nyumba 1500 zilishaunganishwa na matumizi ya gesi asilia .
Amesema matumizi ya gesi asilia ni nafuu zaidi kuliko Nishati nyingine za kupikia ,pia upatikanaji wake ni rahisi ili mradi tu uwe umeunganishwa kwenye miundombinu ya gesi asilia.
“Ukishaunganiswa na gesi asilia ni kama bomba la maji li nakuja nyumbani kwako,unapotaka kutumia maji unaingia jikoni unafungua maji na kuendelea na matumizi yako,ndivyo ilivyo kwa gesi asilia ambapo baada ya matumizi mtumiaji anapata kufunga gesi yake vizuri kwa ajili ya usalama tofauti na mitungi ya gesi,

“Unaweza kutoka kazini umechoka unafika nyumbani gesi imeisha tunaanza kufikiria kwenda kununua,au kuni kuna kipindi kama hiki cha mvua upatikanaji wake ni mgumu  ,pia gesi asilia inasaidia katika utunzaji wa mazingira tunapunguza ukatajibi wa miti ambayo huchomwa kwa ajili ya mkaa au wa ajili kupata kuni.’amesisitiza Mhandisi Gibert