December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nsonda: Miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia wawekezaji tumewekewa mazingira rafiki

Na Esther Macha, TimesMajiraOnline, Chunya

MKURUGENZI wa shule ya Hollyland ,maarufu kwa jina la Lawena Nsonda(Baba mzazi) yenye mchepuo wa kiingereza ya awali na msingi iliyopo katika Mji wa Makongolosi wilaya Chunya mkoani Mbeya , amesema kuwa miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wawekezaji wamewekewa mazingira rafiki ya kufanya kazi na kupelekea ongezeko la wawekezaji toka nje ya nchi .

Nsonda amesema hayo April 14, wakati akizungumzia miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia kuhusu wawekezaji katika sekta binafsi ambapo amesema wamekuwa wakifanya shughuli zao kwa uhuru pasipo kupatwa na changamoto zozote za uwekezaji

“Mama Samia tangia kuingia madarakani tumeona amefanya mambo makubwa hakuna shda kwani tnafanya kaz vizuri ,mtu akikutembelea ofisini kwako kama ni askari au TRA anakuelekeza vizuri kwa maelewano mazuri kujaza taarifa vizuri pamoja na kuweka kumbukumbu tofauti na mara ya kwanza kukimbizana unakua nchini kwako lakini kama hauko nchini kwako unakua kama mkimbzi hivyo kwa upande wa wawekezaji Mama, Samia amefanya kitu ambacho hivi sasa wawekezaji wengi wanafika nchini na kuwekeza na kufanya mambo makubwa tunapongeza sana katika uongozi wake hasa sisi wawekezaji hata kutupigia simu kutuhamasisha tufanye kazi kubwa mfano juzi Mimi juzi Mama Samia kanitumia ujumbe na kunisisitiza kwamba tuzidi kushirikiana kujenga nchi yetu”amesema Nsonda .

Hata hivyo Lawena Nsonda amesema kuwa aliwahi kupokea ujumbe kwanjia ya maandishi kutoka kwa Rais Samia ujumbe huo uliokuwa ukitoa rai kwa wawekezaji kutoa taarifa juu ya changamoto mbalimbali wanazo zipitia katika uwekezaji wao .

Akizungumzia kuhusu uwekezaji wa shule za sekta binafsi amesema kuwa Rais Samia amefanya mambo makubwa kwa kutowasumbua wawekezaji wa shule na hivyo kufanya shule nyingi kujengwa na wamiliki kumsaidia Rais Samia kuhakikisha serikali inawakomboa watoto ambao walikuwa hawafanyi vizuri katika kusoma pia kupitia uongozi wake ameweza kujenga shule za mchepuo wa kiingereza kila wilaya na kuona jinsi gani Rais Samia anathamini sekta ya elimu .

“Kwa pamoja sisi kama wawekezaji tumejaribu kumuunga mkono Mama Samia kuweza kushirikiana nae na kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuinua uchumi wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,lakini tumeona taarifa za mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali akijaribu kuelezea na kuona mapungufu ya hapa na pale kama wabunge wasaidiane na Mama wasimtegeshee katika majukumu yake yote anayoendelea kuyafanya”amesema Nsonda.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya kambikatoto, Christopher Mchaphu amesema kuwa hapo zamani shule za mchepuo wa kiingireza hazikuwepo hivyo alilazimika kuwapeleka watoto wake kwenda kusoma Jijini Arusha lakini hivi sasa mtoto wake mmoja anasoma Hollyland kwasababu ya mazingira mazuri ya shule hiyo ikiwa ni pamoja na taaluma bora.

“Hivyo naomba ndugu zangu wana chunya tuhamasishane tuwalete watoto hapa waje wasome na kupata elimu zamani elimu kama hii tulikuwa tunaona ipo mbali sana , mwanzoni kabisa ilikuwa mpaka uende Nairobi unaweza ukapata shule kama hii badae ikaja mikoa ya kaskazini Arusha na mikoa ya Mbeya wilaya ya Rungwe lakini hivi sasa ipo Chunya hapa ambako ni jirani na ada zake ni za kawaida ambapo ndani yake ni kama kuna msaada fulani “amesema Diwani Mchaphu.

Sophia Mwanauta ni Diwani viti maalum kata ya Makongolosi wilayani Chunya , amesema kuwa uwepo wa shule hiyo katika mji wa Makongolosi ni msaada mkubwa kwa jamii kwani imekuwa kimbilio kwa wazazi walio wengi katika Mji huo kutokana na mazingira mazuri ya kujisomea kwa watoto pamoja maadili mazuri yanayotolewa na uongozi wa shule hiyo ukiongozwa na mkurugenzi wa shule Lawena Nsonda (Baba mzazi).

“Mimi nina kijana wangu anasoma hapa mpaka nimemleta hapa shule hapa nilifanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha utoaji wa elimu niseme ukweli hii shule ni mfano tosha kwa taaluma na maadili kwa watoto, Mkurugenzi wa shule anasimamia vizuri sana shule hii nimpongeze katika hili yupo vizuri “amesema.