November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

SANLG kuwachukulia hatua wanaotumia nembo yao kinyume cha Sheria

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Uongozi wa Kampuni inayojishughulisha na uuzaji wa pikipiki aina ya SANLG wamesema wataendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya kampuni au mtu yoyote ambaye atagundulika kujihusisha na matumizi mabaya ya nembo ya biashara ya SANLG nchini Tanzania

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Route Marketing Consultancy, Anisa Nkulo wakati akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuhusu uuzaji wa pikipiki feki zinazotumia nembo ya SANLG kinyume na sheria za biashara na kanuni.

“Sisi SANLG WORLD INVESTMENT LTD ndiyo wamiliki halali wa nembo ya biashara ya SANLG kama kusajiliwa na BRELA”

Nkulo amesema pikipiki halisi za SANLG zina neno ya SANLG kwenye uma wa mbele wa pikipiki wakati pikipiki feki hutumia lebo za plastiki pekee.

Aidha Nkulo amewataka watanzania wote kutoa taarifa haraka endapo watabaini mtu yeyote nayejihusisha na uuzaji au kutumia pikipiki hizo feki za SANLG ambapo taarifa hiyo ikithibitishwa zawadi nono itatolewa kwa mtia taarifa.

“Tunatoa wito kwa watanzania wote, kutoa taarifa haraka endapo wataona mtu yeyote anauza au anatumia pikipiku feki za SANLG mara taarifa unayotupatia inapothibitisbwa (pamoja na mauzo, anwani ,jina la kampuni , nambari ya mnawasiliano, jina la mhusika na nambari ya TIN), sisi tutatoa zawadi ya shilingi 200,000 za kitanzania”

Kwa upande wake Mratibu mkuu wa Mradi kutoka SANLG, Bahari Leo, amesema Madhara ni mengi kwa kutumia bidhaa isiyo na uhalisia hivyo aliwataka watanzania kuacha kutumia bidhaa feki kwani zinakwamisha maslahi yao katika biashara zao wanazozalisha kwa manufaa ya watumiaji.