November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ukosefu wa vyanzo vya kujiingizia kipato watajwa chanzo cha maambukizi ya VVU kwa mabinti

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Kyela

IMELEEZWA kuwa chanzo kikubwa cha mabinti balehe na wasichana vijana kujiingizia katika maisha hatarishi ni ukosefu wa vyanzo stahimilivu vya kujiingizia kipato na kusababisha kupata maambukizi ya VVU .

Changamoto nyingine mabinti walio kuishi mazingira magumu ,familia zao zimewatelekeza,wengine kufiwa na wanalea ndugu majumbani, wengine wazazi ni wagonjwa na hakuna mtu wa kuwahudumia yote hayo 5yanawafanya wasichague njia zisizo sahihi kujipatia kipato ili kumudu maisha.

Waziri Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera , Bunge na uratibu,Jenister Mhagama amesema hivi karibuni wakati wa kukabidhi mashine za kisasa kwa mabinti kupitia mradi wa Dreams Wilaya ya Kyela.

Mradi huo unaotekelezwa na Shirika la HJFMRI kea ufadhiri wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani PEPFAR kupitia Idara ya Ulinzi ya Marekani nchini ,(WRAIR-DOD)

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,Jaffar Haniu,alisema vitendea kazi vilivyokabidhiwa vitawezesha mabinti kujikomboa kiuchumi na kujiingizia kipato.

Amesema mabinti walio wengi wanalazimika kuingia kwenye mazingira hatarishi kutokana na hali duni za kimaisha walinszo katika familia zao.

Mratibu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids) Emmnuel Petro ,amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri za tatu ikiwepo Jiji la Mbeya na Kyela na Mbarali na kutelekezwa katika Kata 89 zimefikiwa na mpango wa dreams .

Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Frola Luhala amesema tayari wametoa eneo lenye ukubwa wa Ekari 17 kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha kakao na usindikaji kupitia mradi wa huo wa vijana.

Amesema pia wametoa mkopo wa milioni
8 kwa vikundi viwili ili kuwawezesha kujikita katika shughuli za uzalishaji mali na wamepokea maombi ya mkopo wa Sh 36 milioni .

Katika jitihada za kukabiliana na afua za maambukizi ya ukimwi Shirika la kimataifa la HJMRI limetenga Sh 500 kuwezesha mabinti balehe na wasichana vijana kupitia mradi wa Dreams katika mikoa ya Mbeya na Songwe kwa Mji wa Tunduma.

Lengo ni kutekeleza afua za mapambano dhidi ya ukimwi kutokana na kundi hilo kuwa katika hatari kubwa ya kupata maambukizi kufuatia changamoto mbalimbali za utafutaji .

Mkurugenzi Mkuu wa HJMRI Tanzania , Sally Chalamila wamekabidhi vmashine za kisasa za kukamua alizeti ,kutengeza sabuni na vyerehani vya kuweka urembo wa kunakshi kwenye viatu na nguo vyenye thamani ya Sh, 178 milioni .

Vifaa hivyo vimetolewa na shirika la HJFMRI kwa ufadhiri wa Walter Reed Army Institute of Research na Idara ya Ulinzi ya Marekani (WRAIR-DOD) kwa kushirikiana na Asasi ya Tumaini.

Amesema mpango wa dreams umekuwa ukitekelezwa tangu 2016 huku takwimu zinaonyesha mabinti walio katika umri mdogo ni wahanga wakubwa wa maambukizi ya VVU huku chanzo kikiwa ni jitihada za kutaka kujikwamua kiuchumi.

Amesema kuwa tangu kuanza kwa mradi huo mwaka 2016 mabinti 2,661 wamenufaika na mafunzo mbalimbali ikiwepo ushonaji wa nguo, kutengeneza sabuni,matumizi ya kompyuta,utengenezaji wa nywele na ufundi. umeme.

Mwakilishi wa balozi wa Marekani nchini na mtaalam wa masuala ya kuzuia maambukizi kutoka WRAIR -DOD , Dkt. Elick Kayange ,amesema tafiti za kipindi cha mwaka 2016/17 na kurudiwa mwaka 2022/23 matokeo yake yameonyesha mafanikio makubwa ya kuongeza idadi ya watu wanaojua hali za maambukizi na kuanzishiwa dawa.

Amesema ongezeko kwa wale walioanza dawa na kufubaza ni wastani wa asilimia 55.7 mpaka 87.4 huku idadi ya waliotumia dawa na kufubaza VVU imeongezeka kutoka 53.1 mpaka 84.6 kwa mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwepo Mkoa wa Mbeya.

“Licha ya mafanikio hayo kuna kazi kubwa ili kufikia O tatu ifikapo 2030 kusiwe na maambukizi mapya ya VVU wala vifo vitokanavyo na Ukimwi hususan kutokuwepo kwa vitendo vya unyanyapaa na ubaguzi “amesema.

Kwa upande wake mnufaika kupitia mradi wa Dreams, Dorcas Binala amesema kuwa alijiingiza kwenye vitendo vya kujiuza mwili baada ya wazazi wake kupoteza maisha na kujikita kumbeba jukumu la kutunza familia.

Kwa upande wake Mratibu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids) Emmnuel Petro ,amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri za tatu ikiwepo Jiji la Mbeya na Kyela na Mbarali na kutelekezwa katika Kata 89 zimefikiwa na mpango wa dreams .