December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Mfaume:Wauguzi na wakunga Rais Dkt.Samia anawadai

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishena Ustawi wa jamii OR-TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume,amewataka wauguzi na wakunga nchini kutekeleza na kusimamia vyema huduma za uuguzi na ukunga kwani Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anawadai kwasababu ameshaboresha mazingira ya kutendea kazi.

Dkt.Mfaume amesema hayo jijini hapa ,Machi 20,2024 kabla ya kufunga mkutano wa mwaka wa viongozi wa uuguzi na ukunga nchini wenye lengo la kuwaleta pamoja Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya chini na wadau mbalimbali wa Afya kujadili na kupanga mikakati ya pamoja ya namna bora ya kuondoa malalamiko kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma zinazojali utu, heshima, upendo na mawasiliano madhubuti baina ya mtoa huduma na mteja zinatolewa, pia kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa wanafunzi wauguzi katika maeneo ya kutolea huduma za Afya.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatudai wauguzi na wakunga kwani yeye amekwishaboresha mazingira ya kutendea kazi kwa ngazi zote hivyo, tukiwa wauguzi na wakunga tutimize jukumu letu na simamieni vyema huduma za uuguzi,”amesema Dkt.Mfaume.

Aidha alilipongeza Baraza la  Uuguzi na Ukunga kwa kulinda Afya ya jamii kwa kuisimamia vyema Taaluma ya Uuguzi na Ukunga nchini.

“Nimefurahishwa sana na utendaji wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania pia nawapongeza kwa kuadhimisha ya miaka 71 tangu kuazishwa kwa Baraza lakini pia, nikupongeze Msajili wa Baraza Agnes Mtawa, kwa usimamizi mzuri wa kulinda maadili ya kitaaluma hongereni sana Baraza” amesema Dkt.Mfaume

Kwaupande wake Muuguzi Mkuu wa serikali Ziada sella,amesema kuwa ilituwaweze  kuboresha huduma ya jamii inatakiwa kuwa na wauguzi wenye sifa ya kuhudumia jamii, “ni kweli tukubali kuwa tupo na shida ya walimu wasio na sifa ya kufundisha wanafunzi haiwezekani mwalimu umetoka chuo ukaenda kufundisha wanafunzi wakati hujawahi kufanya kazi kwa vitendo,”Sella.

Pia amesema kuwa kuna umuhim mkubwa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania kukaa pamoja na NaCTE na wadau wengine wa elimu ya kuona namna bora ya kuweka utaratibu mzuri wa utoaji mafunzo ya kada ya Uuguzi na Ukunga Tanzania.

“Niwaombe twendeni tukafanye kazi tukifuata miongozo na taratibu huku staha na mawasiliano madhubuti kwa kila mtoa huduma,”amesema Bi.ziada

Awali akitoa salamu kwa mgeni rasmi, Rais wa chama cha uuguzi na ukunga Tanzania Alexander Baluhya  amewataka wauguzi na wakunga kuachana na ubaguzi wa kitaaluma ili kufika mbali katika utendaji 

“Ubaguzi wakitaaluma hautakiwi katika utendaji kazi, tutunziane heshima na mapungufu ya kitaaluma huku tukiitatua migogoro midogo midogo katika tasnia yetu tusikimbilie kwenye vyombo vya habari,”amesema Baluhya.

Naye Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Agnes Mtawa, amewapongeza wauguzi viongozi kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika utendaji wa majukumu ya Baraza katika maeneo yao ya kazi.

“Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa kazi kubwa mnayoifanya huko kwenye maeneo yenu ninyi ni wasaidizi wangu, fanyeni kazi kupunguza malalamiko ya wateja pia simamieni vyema wauguzi watarajali na wale wanao wabeza waleteni huku Barazani tutawashughulikia kwa mujibu wa Sheria,”amesema.