November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sheikh Walid aipongeza Exim bank

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (wa tatu kutoka kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar (watatu kutoka kulia) wakiwa na baadhi ya viongozi wa Exim Bank wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Jaffari Matundu, akizungumza na wadau (hawapo pichani) katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya benki na wadau wake wakiwemo wateja na jamii katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani katika tukio lililofanyika tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi watu, TimesMajira Online

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, ameipongeza Benki ya Exim kwa juhudi zake katika kukuza maendeleo ya kijamii na kueleza shukrani zake kwa mchango wa benki hiyo kwa jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Benki ya Exim pamoja kwa wateja wake iliyofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam Machi 15, 2024.

 Alisema, “Benki ya Exim inaonyesha dhamira ya kweli katika kutumikia wateja wake na jamii kwa ujumla, lengo kuu la Ramadhani ni kuleta watu pamoja, na usiku huu, benki ya Exim imehakikisha kuendeleza lengo hilo kwa vitendo”.

Bwana Jaffari Matundu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, aliwakaribisha wadau wote katika Iftar hiyo huku akitambua mahusiano mazuri ya tija yaliopo baina ya Benki ya Exim na wateja wake na umuhimu wa kuyaendeleza kwa ajli ya ustawi na maendeleo ya jamii.

“Wateja wetu ni zaidi ya wateja tu, ni sehemu muhimu ya familia yetu. Tunaona kila mmoja wenu kama mshirika na mwenzetu katika safari yetu ya mafanikio”, alisisitiza Jaffari Matundu.

Pia, Mkurugenzi huyo alizungumzia hatua na maboresho mbalimbali ambayo yamefanywa na benki ya Exim ili kuendana na mabadiliko katika sekta mbalimbali ikiwemo maendeleo ya teknolojia ya kidijitali na kusogeza huduma kwa wateja.

Jaffari alifafanua kuwa, “tumefanya maboresho makubwa katika mfumo wetu wa Benki ili kuendelea kuhudumia wateja wetu vizuri zaidi kwa kutoa huduma zinazoendana na mabadiliko ya kidigitali”.

“Vile vile tumeendelea kuongeza idadi ya Mawakala wetu (maarufu kama Exim Wakala) ili kuleta huduma zetu karibu na wateja wetu popote walipo”, alimalizia Afisa Mtendaji Mkuu huyo.

Exim Bank pia imeboresha huduma za kidijitali kwa wateja wake ambapo wanaweza kupata huduma za kibenki popote pale walipo ndani na nje ya Tanzania. Hii ni kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa wateja wao na maendeleo ya teknolojia yanayoendelea kutokea duniani.