October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa Idara na vitengo katika banda la Manispaa ya Temeke katika maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba. Na Mpigapicha Wetu

Temeke yatoa mikopo kwa vikundi 100 vya ujasiriamali

Na Penina Malundo, TimesMajira Online, DSM

ZAIDI ya vikundi 100 vimesaidiwa na Manispaa ya Temeke katika kupewa mkopo takribani sh.Bilioni2.4 kwa mwaka wa fedha 2019/20 kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali.

Miongoni mwa vikundi hivyo ni pamoja na kikundi cha Vijana cha Umoja wa Sigara Aggrey Vijana Kazi Tuangoma ambao imewapa kiasi cha zaidi ya sh.Milioni 359 kwa vijana kati ya miaka 18 hadi 35 katika kutekeleza mradi wa ufyatuaji wa matofali .

Akizungumza na Waandishi wa habari Jana jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 44 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba,Ofisa Habari wa Manispaa hiyo Bornwell Kapinga amesema manispaa hiyo imewawezesha vijana hao mkopo usiokuwa na riba ambao inawasaidia katika kuendeleza mradi wao ufyatuaji wa matofali.

Amesema vijana hao wameweza kupatiwa eneo la kufanya biashara,gari la kubeba mbidhaa mbalimbali,Mtambo ya Kisasi wa kufyatulia matofali na wameweza kujengewa Ofisi ndogo kwa ajili ya kufanyia shughuli zao.

“Fedha hizi tuliwawezesha vijana ni fedha za mkopo usiokuwa na ribs unaotolrwa na manispaa yetu na kwa sasa manispaa imesaidia takribani vikundi zaidi ya 100 katika manispaa hiyo,” amesema na kuongeza

“Mwaka wa fedha 2019/20 manispaa ilitenga kiasi cha fedha Bilioni 2.4 kwaajili ya vikundi mbali mbali vya vijana na wanawake huku vikundi 145 vimenufaika na fedha hizi za manispaa,” amesema.

Kapinga amesema manispaa ya Temeke ni tofauti na manispaa nyingine katika utoaji wa fedha za mikopo yao wao wamekuwa wakiwapa watu wanaowaletea maandiko ya miradi na wao kusimamia .

“Tupo tofauti na manispaa nyingine kwani tumekuwa tukitoa mikopo kulingana na maandiko ya miradi na kuhakikisha kikundi kimesajiliwa na uwa kinaanzia watu 10 na kuendelea,” amesema

Kwa Upande wake Muhasibu wa Kikundi cha Umoja wa Sigara Aggrey Vijana Kazi Tuangoma ,Kassim Msongela amesema kikundi chao kinawatu 70 kati ya hao wanne wamepata ajira za moja kwa moja .

Amesema wanaishukuru manispaa hiyo kwa kuwawezesha kwani baadhi ya vijana hao Wapo wengine walikuwa hawana ajira hivyo kuwepo kwa mradi huo kumewasaidia kuwasaidia katika kujipatia ajira.