Na Heri Shaaban , TimesMajira Online
Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Magreth Cheka ametoa msaada wa Baskeli ya miguu Miwili viti mwendo kwa Mtoto mlemavu Leah Ally ili aweze kwenda shule .
Diwani Magreth Cheka alitoa msaada huo leo Kata ya Liwiti wakati ziara yake kutatua kero mtoto Leah (18) ambaye amekosa haki ya msingi ya kupata elimu kutokana na baskeli ya viti mwendo.
“Nilifanya ziara ya kutembelea tawi la Umoja wanawake UWT Liwiti misewe nikapokea changamoto ya Leah mtoto wa mahitaji Maalum alikuwa akiitaji Baskeli ya magurudumu mawili ili aweze kwenda shule leo nimetekeleza ahadi yangu”alisema Magreth
Diwani Magreth Cheka alimtaka Mama mzazi wa Leah kwenda kufatilia shule ili mtoto wake aweze kupata elimu katika shule za Mahitaji maalum zilizopo Wilayani Ilala.
Aidha Magreth Cheka aliwataka wananchi wengine kuunga mkono juhudi zake katika kumsaidia mtoto huyo ambaye anaishi Tabata Liwiti
Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewekeza katika sekta ya Elimu imejenga shule za msingi na sekondari kwa ajili ya jamii iweze kupata elimu .
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt.Samia kwa kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM kwa vitendo na kuongeza fursa mbali mbali za maendeleo katika nchi yetu..
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto