Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Tanga kupitia Hatifungani katika eneo la Mtambo wa Kutibu na Kuzalisha Maji wa Mowe uliopo eneo la Pande, Mkoani Tanga mradi unaokwenda kuongeza kasi ya hali ya upatikanaji wa maji.
Makamu wa Rais akishiriki katika ratiba hiyo amepokelewa na mwenyeji wake Jumaa Aweso Waziri wa Maji.
Mradi huo umelenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi ya uhakika katika maeneo ya Jiji la Tanga, Miji ya Muheza, Pangani na Mkinga wenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 53.12 zitakazopatikana kupitia uuzaji wa Hatifungani ya Kijani ya Tanga UWASA na unatarajiwa kutekeleza ndani ya mwaka mmoja kuanzia Aprili, 2024.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi