Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina amani, umoja, mshikamano na utulivu pamoja na kuendelea shughuli za kimaendeleo na ibada.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo akizungumza alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa na kufungua Ijitimai ya Kimataifa Tabligh Markaz Magome ya siku tatu Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe: 02 Februari 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amewataka waumini kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa waumini kuwafundisha watoto elimu ya dini ili wawe na hofu ya Mwenyezi Mungu kwa kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na vitendo vya udhalilishaji .
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kuratibu vizuri shughuli za dini kwa utulivu, amani na mshikamano.
Matukio mbalimbali katika picha
More Stories
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania