November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Matokeo ya Kihistoria yenye kugusa maisha ya watu, jamii na uchumi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Leo, Benki ya NMB tumetangaza matokeo ya kiutendaji ya mwaka 2023, yakionesha kuvunja rekodi kwa mwaka mwingine tena baada ya kupata mafanikio ya kihistoria.

Kati ya mengi, tumeweza:

➡️ Kuongeza Jumla ya mapato ya Benki na kufikia Shilingi Trilioni 1.4 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18 mwaka hadi mwaka.

➡️ Uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato uliboreshwa zaidi hadi kufikia asilimia 39, wakati uwiano wa mikopo chechefu umeshuka hadi kufikia asilimia 3.2. Takwimu hizi zote ni chini ya ukomo wa kikanuni wa Benki Kuu wa asilimia 55 na asilimia 5 mtawalia.

➡️ Kutokana na ufanisi huu, Faida kabla ya Kodi imeongezeka kwa asilimia 26 hadi Shilingi Bilioni 775 huku Faida baada ya Kodi ikifika Shilingi Bilioni 542 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 kwa mwaka. Hiki ni kiwango kikubwa cha faida na cha kihistoria kwa Benki ya NMB na sekta nzima ya fedha nchini.

➡️ Mizania ya Benki imeendelea kukua na kufikia jumla ya mali ya Shilingi Trilioni 12.2 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 19 kwa mwaka.

➡️ Tuliendeleza ajenda ya ujumuishaji wa kifedha kwa kufungua akaunti mpya za wateja zaidi ya milioni 1.2, na kufanya jumla ya akaunti za wateja wetu kufikia zaidi ya akaunti milioni 7.1. Hii ni idadi kubwa zaidi ya wateja kwa taasisi moja ya fedha nchini.

➡️ Tuliwekeza zaidi ya Tsh Bilioni 6 kwenye elimu, afya na mazingira, ikiwa sehemu ya dhamira yetu ya kujitolea kusaidia jamii inayotuzunguka.

Akiwasilisha Taarifa ya Fedha ya Mwaka 2023, Afisa Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna amewashukuru wateja wetu, wanahisa, wafanyakazi, washirika wote wa Benki, Serikali kupitia Benki Kuu na Watanzania wote kwa mchango wenu thabiti na imani mliyonayo kwa Benki ya NMB.