November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wamiliki 10 wa Malori walipwa fidia

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

WAMILIKI 10 wa Malori Tanzania wamelipwa fidia baada ya takribani miaka nane kupita tangu malori yao kuungua huko Kasumbalesa nchini Kongo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Elius Lukumay amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

‘’Takribani miaka 8 iliyopita baadhi ya wamiliki ya malori Watanzania waliunguliwa na magari yaliyokuwa sehemu ya maegesho huko Kasumbalesa Kongo leo wamiliki 10 wamepata malipo yao,’’amesema Lukumay.

Amesema kuwa kati ya hao kumi waliolipwa fidia zao nane wapo hai na wemeshaanza kulipwa wengene wawili walifariki hivyo wanaendelea na mchakato wa kutafuta familia zao kwa ajili ya kukawakabidhi taratibu za fidia zao.

Ameeleza kuwa katika maegesho hayo jumla ya magari 100 yaliteketea kwa moto, kati ya hayo malori yanayomilikiwa na Watanzania yalikuwa 36.

‘’Awa 10 wamelipwa malipo yao kwasababu walikidhi vigezo lakini kuna wale waliokuwa na bima kubwa walilipwa kipindi kile kile, kuna wengine walikuwa na bima feki,’’amesema


Likumay amesema miongoni mwa sababu zilizosababisha malipo hayo kuchelewa ni kwasababu magari hayo yaliungua nje ya Tanzania.

‘’Tulijitahiji kushurikiana na walishirikiana na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwasababu wengi walikuwa wamekata bima zao hapo,’’ amesema.

Pia amewashauri wamiliki wa malori kutambua umuhimu wa kuwa na bima halali ili kuwasaidia kutoanguka kiuchumi mara baada ya majanga kutokea.

Aidha amesisitiza kuwa malipo hayo ni kwa ajili ya magari na si mtu mmoja mmoja.

Meneja wa Masoko wa NIC, Karimu Meshack amesema ni wakati muafaka wa wamiliki wa magari wa kushirikiana na Taasisi za bima pindi wanapohitaji kukata bima ili kupunguza kuchukua muda mrefu kwa ajili ya malipo endapo majanga yakitokea majanga.

Pia amewata madereva na wamiliki wa magari kuhifadhi nyaraka zao hata ambazo zimetolewa ya taarifa zao ili ikitokea changamoto ziwasaidie ili kuharakisha malipo yao.

Mmiliki wa kampuni ya Heaven logistic, Deigratias Mitile ameishukuru Tatoa pamoja na NIC kwa kukamilisha malipo hayo na kuwasihi wamiliki wa magari wengine kutopuuzia kukata bima halali.

Naye msimamizi wa Kampuni ya vigu Trading, Eva Mkomba ameishukuru serikali na Tatoa kwa kusimamia na kuhakikisha wanalipwa fidia zao.