November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbemenda ajenga ofisi ya CCM Chanika Tungini

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Tungini kata ya CHANIKA Wilayani Ilala,Yusuph Memenda , amejitolea kujenga ofisi ya chama cha Mapinduzi CCM Tungini kwa ajili ya kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi na CCM

Mwenyekiti Yusuph Mbemenda alisema hayo wakati wa kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani kazi zilizofanywa na Serikali ya mtaa Tungini toka mwaka 2019 mpaka Desemba 2023 ambazo zimesimamiwa na Mwenyekiti Yusuph mbele ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Tawi La Tungini.

Akizungumza katika kikao cha kuwasilisha taarifa ya kazi Mwenyekiti Yusuph alisema wakati anaomba uongozi wa Serikali za mitaa alitoa ahadi mbali mbali ambazo alitoa ahadi kuzitekeleza ikiwemo kujenga ofisi ya CCM.

“Tunajenga ofisi ya CCM tawi la Chanika Tungini, ambayo itakuwa na Ofisi ya chama na Jumuiya pamoja na ukumbi wa mikutano ya chama sehemu ya kazi nilizotekeleza katika uongozi wangu ambapo leo tunakabidhi vifaa vya ujenzi saruji,Mchanga,Nondo,kokoto kwa ajili ya kumaliza ujenzi wa jengo la chama”alisema Yusuph.

Mwenyekiti Yusuph alisema changamoto zingine ni barabara za mitaa wanajenga vivuko katika uongozi wake ambao yupo madarakani kwa kushirikiana na Chama na Serikali .

Akizungumzia hali ya Usalama alisema hali ya ulinzi na Usalama nzuri wanashirikiana na Jeshi Jeshi la Polisi katika kuimarisha Ulinzi kila siku.

Aidha Alisema katika maendeleo changamoto azikosekani zoezi la Serikali la Anuani za makazi post kodi baadhi ya nyumba hawana anuani za makazi wanaendelea kuwapa elimu ili wananchi wote wa Mtaa Tungini waweze kulipia namba za nyumba

Mwenyekiti wa CCM Tawi la Chanika Tungini Rajabu Magimbi alipongeza Uongozi wa Serikali za mitaa Chanika Tungini kwa kufanya jambo kubwa ndani ya chama ambapo alisema leo ni siku ya historia kwa Serikali ya Mtaa Tungini kufanya jambo kubwa CCM ambapo akitaka viongozi wengine wenye mapenzi mema ya chama kuiga mfano.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Chanika Tungini Zahara Njaidi alitumia nafasi hiyo kupongeza Serikali ya Mtaa huo na Wajumbe wake kwa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani kuelezea kazi walizofanya katika uongozi wao.

Katibu Zahara aliwataka wadau wa Chama cha Mapinduzi kujitokeza kuwaunga mkono ili kumalizia jengo hilo hatua ya Bati iliyobaki ili ofisi iweze kutumika ya chama cha Mapinduzi CCM.

Aidha alimuomba Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde kuwaunga mkono kumalizia ujenzi huo hatua ya mwisho ambapo bado milango ,mabati na madirisha .