Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na watoto Riziki Pembe Juma ameipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa Kazi kubwa waliyoifanya ya kuingizia faida ya Bilioni 78 Kwa mwaka 2023 kulinganisha na Bilioni 22 Kwa mwaka 2022 Jambo ambalo litasaidia kuipatia gawio kubwa Serikali.
Akitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar, (PBZ) huko Nungwi Wilaya ya Kaskazini ‘A,’ Unguja ikiwa ni miongoni mwa Shamrashamra ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Amesema mafanikio hayo yanatokana na miongozo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kupitia Wizara ya Fedha na Mipango Kwa kusimamia na kujenga vianzio vingi vya fedha.
Aidha amesema Benki hiyo imeweza kutoa mikopo ya Trilioni moja Kwa wateja wake na kuendeleza kuwa kiungo muhimu katika Taifa, ndani ya Zanzibar na Tanzania Bara kiujumla.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Dkt. Juma Malik amesema Sera miongozo pamoja na busara ni matokeo ya viongozi wakuu wa nchi mbili yenye lengo la kuhakikisha wanawaletea maendeleo wananchi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Said Mohammed Said amesema kimtandao Benki hiyo imekuwa Kwa kasi sana ambapo katika mwaka 2020 ilikuwa na matawi 29 Kwa muda wa miaka mitatu kumekuwa na matawi 46, mwaka 2023, vikiwemo vituko 35 Zanzibar na 11 kwa Tanzania bara.
Amefahamisha kuwa Benki ya Watu wa Zanzibar ni taasisi ya kifedha inayomilikiwa na wananchi pia ni miongoni mwa matunda ya Mapinduzi ambayo imeanzishwa ndani ya miaka miwili baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Kwa hivi sasa inatimiza miaka 58.
Kwa Upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja Rashid Hadid Rashid amewataka wananchi wa Nungwi kuitumia Benki hiyo Kwa kulipia malipo ya Serikali, kubadilisha fedha za kigeni pamoja na kufungua akaunti kwa kuweka na kutoa fedha ili kuziweka katika sehemu salama.
Â
Amewataka wafanyakazi wa Benki hiyo kutoa taaluma ya matumizi ya Fedha Kwa wajasiriamali ili kupatiwa Elimu, mitaji na masoko pamoja na punguzo la masharti ya mkopo kutokana na hali zao ili dhamira ya Rais wa Zanzibar ya kuwapatia maendeleo ifikiwe.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi