Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tabora wamempongeza Rais wa awamu ya 6 Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za afya kwa kiasi kikubwa kama ilani ya uchaguzi ya chama inavyoelekeza.
Tamko la pongezi hizo limetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Tabora Robert Elieza Kamoga alipokuwa akifungua katika kikao cha Baraza la Wazazi Mkoa kilichofanyika juzi katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini hapa.
Amebainisha kuwa
Jumuiya hiyo imeridhishwa na kasi ya Mheshimiwa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa ya kujenga
miundombinu ya afya katika wilaya na Mikoa nchini kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Aidha amempongeza kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga idadi kubwa ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, vyumba vya maabara, nyumba za walimu, maktaba na maabara katika shule za sekondari.
‘Maboresho haya yanaonesha ni kwa kiasi gani Rais Samia anavyotekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, katika hili tunampongeza sana,’ amesema.
Kamoga amebainisha kuwa maboresho hayo yameleta tija kubwa katika sekta ya afya na elimu kwani changamoto zilizokuwepo zimepungua kwa kiasi kikubwa.
Kama Jumuiya ya Chama tutaendelea kuunga mkono juhudi zote zonazofanywa na Mheshimiwa Rais katika kuwaletea maendeleo wananchi,’ amesema.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoani hapa Emanuel Sabuhoro amewataka Watendaji na Viongozi wote wa Jumuiya hiyo kuendelea kusimamia vema utekelezaji majukumu yao ili kuharakisha maendeleo ya jumuiya hiyo.
More Stories
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja
Gavu aanika miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita Geita