Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mwenyekiti wa umoja wanawake UWT Mkoa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo amewataka UWT Wilaya ya Ilala kuongeza wanachama wa jumuiya ya wanawake.
Mwenyekiti wa UWT mkoa Mwajabu Mbwambo , aliyasema hayo Tawi la Kivule Mashariki wilayani Ilala wakati wakati wa kuzindua mashina vizimba vya umoja wanawake UWT pamoja na kupokea wanachama wa UWT wapya kivule Mashariki.
“Dar es Salaam mwaka 2023 wameongeza wanachama wa UWT wapya 45,046 ukilinganisha na idadi ya wanawake wote ndani ya mkoa huu zaidi ya milioni 2 katika takwimu za sensa ya Makazi ya watu “,alisema Mwajabu.
Mwenyekiti Mwajabu ameagiza matawi yote ya UWT wilaya ya Ilala kuongeza wanachama wapya ili kujenga Jumuiya ya wanawake iweze kusonga mbele katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi
Amesema Jeshi la Wanawake ni jeshi kubwa ambapo aliwataka washirikiane pamoja katika kujenga chama na jumuiya kukiaiikishia CCM ina shika dola katika chaguzi zake zote ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.
Amewaomba viongozi wa matawi wa UWT kujenga mahusiano mazuri na taasisi zinazowazunguka ikiwemo shule na vyuo kwa ajili ya kusajili wanachama wa UWT kuanzia miaka 18 kuendelea kwani wapo wengi wapite kuvuna wanachama .
Aidha katika hatua nyingine amewataka wanawake wachukue fomu za uongozi kugombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ukifika wakati mwaka 2024 wana haki ya kugombea .
Akizungumza na wanawake wa UWT Kivule amesema siasa na Uchumi aliwataka UWT kivule kuwa wabunifu katika kubuni miradi ya jumuiya ya wanawake waweze kujikwamua kiuchumi .
Amewataka UWT Kivule kumtumia Diwani wao wa Viti Maalum Eva Nyamoyo ambaye ni mlezi wao katika shughuli za Jumuiya hiyo ikiwemo kubuni miradi ya biashara zao ili waweze kusonga mbele.
Katika hatua nyingine amezungumzia vitendo vya ukatili wa kijinsia amewataka wanawake wa UWT kukemea vitendo hivyo kwa watoto wao majumbani ambapo aliwataka wanawake kusimama imara nyumbani Baba atakuwa kichwa cha Familia na Mama ni mlezi wa familia.
More Stories
Samia apeleka neema Tabora, aidhinisha Bil. 19/- za umeme
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe