Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Kinondoni
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Dar es Salaam Janeth Masaburi amempongeza Wakala Barabara nchini TARURA Wilaya ya Kinondoni kwa kujenga Barabara vizuri.
Mbunge Janeth Masaburi alitoa pongezi hizo wakati wa Kufanya ziara wilayani Kinondoni kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuhamasisha matumizi ya Nishati ya gesi kwa kutoa elimu kwa wanawake.
“Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa pesa nyingi katika miundombinu ya Barabara ujenzi wa barabara hii ya Nyota njema ya kiwango cha lami Km 1 .4 imefikia asimilia 97 “alisema Masaburi.
Aidha Mbunge Masaburi ameomba Serikali Dar es Salaam waongezewe fedha kutokana na ukubwa jiji hilo la Biashara la uchumi kutokana na kufanyika Biashara nyingi.
Wakati huo huo Mbunge Masaburi amewataka wananchi wa mkoa Dar es Salaam kutumia nishati ya gesi na mkaa mbadala waache kutumia mkaa na ukataji misitu wanaharibifu wa mazingira .
Aliwataka wanawake wa soko Kunduchi Pwani ,na Kawe kwa Mwaiposa watumie Nishati ya gesi waweke pesa katika vibubu waweze kununua majiko ya kisasa ya gesi .
Kwa upande wake Mhandisi wa TARURA wilayani Kinondoni Queen Nyigu alisema barabara ya Nyota Njema ina urefu wa KM 1.4 barabara ya kiwango cha lami na miundombinu ya mifereji na zege ambapo chanzo cha fedha za mradi ni fedha maalum za mfuko wa Barabara kwa mwaka wa fedha 2022 /2023.
Mhandisi Queen Nyigu alisema ujenzi huo unakadiriwa kugharimu kiasi cha fedha jumla ya shilingi bilioni 1.8 ambao unajumuisha ujenzi wa miundombinu ya kutoa maji ya mvua ,taa za Barabara, pamoja na barabara za kiwango cha lami.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa