November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani amuunga mkono Samia katika michezo

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Dwani wa Kata ya Upanga MASHARIKI Sultan Salim, ameunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya michezo kwa kutoa vifaa vya michezo bure katika vyuo vya Serikali CBE, DIT na Elimu ya Watu Wazima wilayani Ilala

Akikabidhi vifaa hivyo kwa vyuo vitatu Chuo cha Dar es Salaam Instute of Teknology ,College Bussiness Education na chuo cha Elimu ya Watu Wazima alisema anaunga mkono juhudi za Rais Samia kukuza sekta ya michezo mwende mkafanye vizuri katika mashindano ya vyuo vikuu vya Kati Tanzania mashindano ambayo yanafanyika Mkoani Iringa Desemba mwaka huu 2024.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapenda michezo katika nchi yake Tanzania amekuwa akitoa hamasa na kusaidia klabu zetu kufanya vizuri za Simba ,Yanga na Timu ya Taifa Star katika mashindano ya makombe mbalimbali na sisi wasaidizi wake tunaunga mkono juhudi zake sehemu ya kutekeleza Ilani kwani michezo ni afya pia ujenga mahusiano na udugu pia michezo ni ajira “alisema Sultan.

Diwani Sultan alisema katika kuunga mkono juhudi za Serikali sekta ya michezo ni endelevu anafanya kusaidia vyuo hivyo vitatu ,CBE,DIT na chuo cha Elimu ya Watu ya watu wazima waweze kwenda kufanya vizuri mashindano yao ya vyuo vikuu .

Diwani Sultan Salim alisema kampeni hiyo ni endelevu ana mapenzi makubwa na vyuo hivyo kuvisaidia kwani ni chimbuko la vijana wengi katika serikali hii wamekuwa viongozi mbalimbali wa chama na Serikali .

Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha College Bussiness Education CBE Khalifa Khalifa alimpongeza Diwani Sultan kwa msaada wake huo wa vifaa vya michezo mpira na jezi kwa timu zote za wanawake na wanaume ambapo alisema wamejiandaa vizuri wapo tayari kwa ajili ya safari mkoni Iringa katika mashindano ya vyuo vya kati nchini .

Katibu wa Seneta Mkoa Dar es Salaam Mabula Marco Mabula alivitaka vyuo vya CBE na DIT kutoa ushirikiano chama na Serikali kwa wanafunzi wanaowaongoza katika vyuo hivyo ,Viongozi walioshindwa kutoa ushirikiano katika vyuo hivyo wakae Pembeni.