Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) leo tarehe 1 Desemba, 2023 umeshiriki Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Michezo vya Shule ya Sekondari Morogoro. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2023 yamebeba kauli mbiu isemayo “Jamii iongoze kutokomeza UKIMWI”.
More Stories
Muhoji Sekondari kumaliza changamoto ya umbali kwa wanafunzi Musoma vijijini
Tanzania mwenyeji mkutano wa nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika
TANESCO yarudisha shukrani kwa jamii