Na Mwandishi wetu
SERIKALI kwa kushirikiana na wadau kutoka nchi ya Hamburg ,wameonyesha dhamira ya uboreshaji wa bustani mbalimbali zilizopo katika miji ikiwemo mji wa Dar es Salaam ambao itawasaidia kuongeza pato ya nchi kwa kupitia watalii wanaoingia nchini.
Akizungumza Jana wakati wa uzinduzi wa warsha ya uboreshaji wa Bustani ya Botanical iliyopo Dar es Salaam Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Majura Mtalemwa, amesema wataalam kutoka jiji la Hammbarg nchini Ujerumani wamefika nchini kwa lengo la kusaidia utoaji wa elimu na jinsi ya kuendesha bustani.
Mtalemwa amesema uboreshwaji wa Bustani hizo ni chachu kubwa ya kuja kuongeza mapato kwa taifa kwani watu watakuwa wanafika katika maeneo hayo na kupumzika au kuangalia viungo mbalimbali ambavyo vimepandwa katika Bustani hizo.
Amesema miaka mingi bustani hizo zilikuwa zinaendeshwa bila ya kuingiza faida yeyote,hivyo ushirikiano huo utasaidia na kuongeza chachu kwa Jamii kufika katika maeneo hayo kupumzika au kujisomea kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mali kale ya Makumbusho Rivocatus Ligumba amesema eneo la bustani Botanical ni eneo la kihistoria toka enzi za zamani.
Amesema maeneo ya bistani muhimu duniani kote kwa sababu zina historia nyingi ambazo ni faida kwa vizazi vijavyo.
“Eneo kama hili wanafunzi wanakufa nakufanya masomo yao kwa vitendo kwa kujua mti fulani unafaida gani? Na nini chimbuko lake,”amesema
Naye, Seneta kutoka mji wa Hamburgn anaeshughulikia masuala yanayohusu nchi ya Afrika,Dkt Anna Catarina Seboda amesema wanamahusiano mazuri na Tanzania tangu miaka 12 iliyopitia katika masuala mbalimbali ikiwemo kupeana uzoefu wa jinsi ya kutunza bustani na miji.
Amesema hivi sasa wamekuja na wataalam wao ambao kazi kubwa itakuwa ni kuboresha bustani ya botanical kwa lengo la kuongeza pato nchini na kuongeza kasi ya Watalii nchini.
Amesema si kuongeza pato peke yake ila bustani hiyo ikifanyiwa ukarabati watu wengi zaidi watafika kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo miti iliyopo ndani ya bustani hiyo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi