Na IsraelMwaisaka, TimesMajira Online, Sumbawanga
MKAZI wa kijiji cha Muze kilichopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga Edward Silungu (32) amekufa papo hapo baada ya kupigwa radi iliyoambatana na mvua kubwa.
Edward alifikwa na umauti akiwa amejikinga na mvua chini ya mti akiwa na baba yake mzazi Ibrahim Silungu (75) ambaye hakujeruhiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukie amethibitisha tukio hilo ambalo lilitokea Jumatatu asubuhi.
Kufuatia mkasa huo amewataadharisha wananchi kuchukua tahadhari katika msimu huu wa Masika kwa kutokimbilia kukaa chini ya miti.
Katika tukio lingine lilitokea Jumatatu asubuhi , Mkuu wa Wilaya Chirukie amethibitisha kuwa ng’ombe 27 wamekufa baada ya kupigwa na radi huku wengine wawili wakiwa wamejeruhiwa .
Akizungumza na wanahabari jana jioni Chirukie amesema vifo vya ng’ombe vilitokea katika maeneo mawili tofauti katika Manispaa ya Sumbawanga katika kijiji cha Tamasenga ambapo walikufa ng’ombe 25 huku wawili wamejeruhiwa.
Huku katika kijiji cha Muze kilichopo katika Bonde la Ziwa Rukwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wamekufa ng’ombe wawili .
” Ng’ombe wapatao 78 ambao mali ya mfugaji mmoja wakiwa zizini ghafla radi ilipiga na kuuwa 25 ,wawili wakiwa wamejeruhiwa huku 53 hawakujeruhiwa ” alieleza
Aliongeza kusema kuwa ” Nimeamuru mizoga hiyo iteketezwe na kuzikwa chini ya usimamizi wa wataalamu wa mifugo na viongozi wa eneo hilo” alisisitiza.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa