Na Moses Ng’wat,Timesmajiraonline,Songwe.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, atafanya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Songwe kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo, kuongea na wananchi pamoja na watumishi wa umma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 20 2023, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael amesema kuwa, Waziri Mkuu atawasili mkoani Songwe Novemba 22, 2023 na atahitimisha ziara yake Novemba 25, 2023 ambapo atetembelea Wilaya mbili za Ileje na Mbozi.
Dkt.Francis amebainisha kuwa Novemba 23, 2023 Waziri Mkuu atakagua miradi miwili, kuweka mawe ya msingi ya miradi miwili pamoja na kuongea na wananchi Wilayani Ileje.
Dkt. Francis ameongeza kuwa Novemba 24, 2023, Waziri Mkuu atakuwa Wilayani Mbozi ambapo atazindua mradi mmoja, kukagua miradi miwili, kuweka Howell la msingi mradi mmoja pamoja na kuongea n wananchi.
Amebainisha kuwa siku ya Novemba 25, 2023 Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara yake, ikiwa ni pamoja na kuongea na watumishi wote wa Mkoa wa Songwe ambapo majumuisho hayo yatafanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Dkt. Francis ameeleza kuwa ziara hiyo ya Waziri Mkuu Mkoani humo ni muendelezo wa ziara aliyoifanya Aprili 13 hadi 16 , 2023 ambapo alitembelea Halmashauri tatu za Momba, Songwe na Tunduma.
Aidha, Dkt. Francis ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kumpokea Waziri Mkuu .
More Stories
TAKUKURU,rafiki yanufaisha wananchi Mwanza
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa