November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa Mkoa, CCM Mbeya kumlinda Dkt. Tulia

Na Esther Macha, TimesMajira Online, Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, amwaonya watakaojitokeza kuwania kiti cha Ubunge Mbeya Mjini katika uchaguzi mwaka 2025, huku Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoani humo kikiahidi kumlinda Rais wa 31,wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye ni Spike wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Askson.

Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na viongozi wa Chama na Serikali katika mapokezi ya Spika wa Bunge na Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe, jijini hapa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kama Serikali wataendelea kumlinda jua liwake mvua inyeshe katika uchaguzi Mkuu 2025.

“Nashangaa wapo watu ambao wanatoa lugha za kumtukana Dk Tulia tena mpaka makanisani kwa kweli hilo halikubaliki na hatupo tayari kurejea kipindi cha miaka 10 tuliyopitia katika jimbo la Mbeya”amesema Homera.

Amesema kwa kipindi kifupi Mkoa wa Mbeya umepiga hatua za maendeleo hususan katika nyanja za Afya,maji na miundombinu ya barabara njia nne”amesema.

Kwa upande wake Mbunge viti maalum Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Maji mhandisi,Maryprisca Mahundi amesema Dkt. Tulia amewaheshimisha sana wanawake Mkoa wa Mbeya kwa ushindi wa kishindo .

“Tunafuraha kubwa kwa Dkt.Tulia kutuheshimisha wana Mbeya wanawake tunaweza tunasimama na Dkt.Tulia  tunasema asante Sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan umetupa heshima kubwa wana Mbeya,naomba wanawake wote tuendelee kushikamana kwa pamoja “amesema Mhandisi Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Mbeya.

Naye Mjumbe wa halmashauri Kuu Taifa(NEC) Mkoa wa Mbeya,Ndele Mwaselela,amesema kuwa Dkt .Tulia ameliheshimisha Taifa kwa kupata kwa kishindo nafasi ya urais wa 31 wa Mabunge Duniani (IPU) na kwamba ulifika wakati wa Mungu kwa nchi ya Afrika.

“Mh Rais akukosea kumtuma Dkt. Tulia Ackson kugombea nafasi ya IPU na kama chama wanatoa ahadi ya kumlinda na kuhakikishia ushindi wa kishindo katika nafasi Rais na Ubunge Oktoba 2025”amesema.

Christopher Uhagile ni Katibu Mwenezi wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Mbeya, amewataka wana mbeya kupendana ikiwa ni pamoja kumpa ushirikiano Dkt.Samia pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.