November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kitabu cha kuanzisha, kuratibu Klabu za Kidigiti chazinduliwa

Mwandishi wetu, Timesmajira online

SERIKALI imezindua kitabu cha kuanzisha na kuratibu Klabu za Kidigiti Kwa lengo la kusaidia vijana kuongeza bunifu na ujuzi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Novemba 2, 2023 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mohammed Khamis Abdulla amesema kwa mara ya kwanza Serikali inaandika historia Kwa kizindua kitabu Cha kuanzisha na kuratibu klabu za kidijiti.

“Nitoe wito kwa wakuu wa shule za Serikali, binafsi na vyuo kuhamasika kuanzisha Klabu hizi za Kidigiti na kuhakikisha wanazisimamia na kufuata maadili,” amesema Abdulla

Amesema kuzinduliwa kwa Kitabu hicho ni katika kuhakikisha wananchi, hususan Vijana wanashiriki katika uchumi wa Kidigiti.

“Kuzinduliwa Kwa klabu hizi za kidijiti kutawezesha Vijana kujifunza na kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya kidigitali wakiwa katika umri mdogo kwani Klabu hizi zitaanzia ngazi ya shule za awali, naingia, Sekondari na vyuo vikuu.

Aliongeza kuwa Klabu za Kidigiti zitawajengea Vijana fikra chanya zitakazowasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili pamoja na kuwasiadia katika uchumi wa Kidigitili na kupata ujuzi.

Aidha amesema kuwa katika mkakati wa kidigitali wa Mwaka 2023 Serikali imeainisha kuwa inataka kuwa na jamii ya kibunifu.

Vilevile amesema Kitabu hicho kitakuza tamaduni ya kibunifu nchini na kujenga jamii imara ya kibunifu.

“Ili kupata jamii yenye kushiriki uchumi wa kidigitali ni lazima kuwekwa kwa Mazingira bora ya ushiriki.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Dk.Jabir Bakari amesema klabu za kidijiti ni majukwaa ya hiari yanayowakutanisha wanafunzi wa rika moja kupata uelewa na kuhamasishana juu ya tehama.

“Kupitia klabu hizi za kidijiti tunajenga jamii yenye ufahamu wa teknolojia ya kidijiti na iliyo na taarifa na fursa zake “amesema Dk.Bakari .

Aliongeza kuwa dunia ipo katika zama za taarifa zinazoenda sambamba na uchumi wa kidijiti .

Aidha amesema katika zama hizi ambazo zinajulikana kama zama za mapinduzi ya nne ya viwanda tehama ndiyo nyezo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, Dkt Jabir Bakari akizungumza katika hafla ya Uzinduzi huo
Katibu Mkuu wa wizara ya habari mawasiliano na Teknolojia ya habari, Mohammed Khamis Abdulla akizungumza katika hafla hiyo ya Uzinduzi kitabu cha kuanzisha na kuratibu klabu za kidijiti