November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Sekondari Viwege wajivunia mafanikio kitaaluma

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Shule ya Sekondari Viwege Kata ya Majohe wilayani Ilala,wajivunia mafanikio kitaaluma kwa miaka mitatu mfululizo inafanya vizuri.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa shule ya Viwege Ilala Sifa Said Mwaruka, katika mahafali ya 13 ya kidato cha nne ya shule hiyo ambapo wanafunzi 306 waliitimu wavulana 154 na wasichana 152.

“Shule yetu ya Sekondari Viwege maendeleo ya kitaaluma kwa shule yapo vizuri ambapo mwaka 2020 ,2021 na 2022 imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo yake kitaaluma ambapo kidato cha nne mwaka huu tunatarajia kufanya vizuri zaidi “alisema Mwaruka.

Mkuu Sifa Said Mwaruka, alisema matokeo ya kidato cha nne wana uhakika yatakuwa mazuri maana yanaenda yakipanda yaani pre NECTA na mkakati wa kuondoa ziro wanatimiza kwa vitendo na kuleta matokeo chanya ya kitaaluma.

Akieleza mafanikio katika shule ya viwege amesema wamejengewa madarasa kumi ya COVID19,na pochi la mama kwa mwaka 2020 ,2022 yenye thamani ya shilingi milioni 200 ,wamejengewa mahabara ya kisasa za Chemistry ,Biology,na physics,kwa fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kufuatia mahabara ya awali kuungua moto .

Pia amesema wamejengewa Hosteli ya wasichana na ofisi ya kisasa ,wamewekewa mazingira bora ya kujifunzia na kudhibiti utoro kwa kushirikiana na polisi Jamii .

“Shule yetu ipo Majohe wilayani Ilala ilianza mwaka 2007 haya ni mahafali ya 13 idadi ya wanafunzi wa shule nzima 1449 ,shule ina idadi ya madarasa 36 pongezi kubwa zimwendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea madarasa manne ya kisasa na madarasa sita ya pochi la Mama “amesema.

Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Semeni Mtoka, amewapongeza wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo na kuwataka waendeleze mazuri ya shule hiyo wawe mabalozi huko waendako wasishawishike kuingia katika makundi yasiofaa badala yake wawe na nidhamu waliofundishwa viwege sekondari.

Amewataka Wazazi kuwalea watoto katika misingi mema wasiingie katika mmomonyoko wa maadili huku wakijiandaa kwenda vyuo mara baada matokeo yao kutangazwa ya kidato cha tano.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Majohe AMINA KAPUNDI, amepongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta ya Elimu kuwajengea mahabara ya kisasa shule hiyo ,pia alipongeza Serikali kuwapelekea Maji ya DAWASA Majohe na Umeme wa Vijijini mradi wa REA wa shilingi 27,000/= wananchi wanafurahia matunda ya Serikali yao katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM wamenufaika.