Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wanafunzi waliosoma shule ya Tanga school Alumni Association kuweka mikakati ya kitaaluma iwe shule bora katika ufaulu Tanzania.
Raia Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, alisema hayo wakati wa uzinduzi wa mkutano mkuu wa umoja wa wanafunzi waliosoma Tanga school (TSAA)
“Umoja wa Shule ya Tanga school wanazingatia ubora wa elimu kwa kuweka mazingira bora ya shule kwa kuwekeza katika maktaba wengi tumesoma Tanga mikakati yetu umoja uwe na nguvu baada miezi mitatu tukutane tena kwa ajili kutoa michango na kuendeleza shule yetu “alisema Kikwete.
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alisema mikakati yao mingine wanafunzi waliosoma Tanga school TSAA Shule hiyo ingie katika hesabu ya shule bora ya ufaulu Tanzania.
“Mimi ni miongoni mwa mwanafunzi niliosoma Tanga school nilijiunga mwaka 1970 nikatoka mwaka 1971 baada kutoka mwaka huo alirejea tena mwaka 1987 kutembelea shule hiyo na viongozi wengi wa Serikali wakiwemo Majaji walisoma shule hii”alisema.
Mwenyekiti wa umoja Wanafunzi wa Tanga school Meja Generali Mstaafu Hamisi Semfuko alisema haikuwa kazi rahisi kukusanya dhamira za waliosoma miaka ya 1960 na kuziunganisha na dhamira za vijana wa sasa waliopita Tanga school mpaka kufikia kuunda Taasisi rasmi iliyoweka malengo ya kuiangalia Tanga School kwa jicho la dhamira moja .
Meja Generali Mstaafu Hamisi Semfuko amesema mafanikio ya jambo hili ni zawadi kubwa ,kubwa kwa kizazi kijacho na Taifa letu na sio Tanga School ambapo alimshukuru Mwalimu Zuberi Mohamed kwa jitihada yake kubwa ya kufanya utafiti wa historia nzima ya Tanga school na kutumia muda wake kuisumilia ni matumaini yetu kuwa ataendeleza jitihada hizo na kufikia kuandika kitabu cha historia ya Tanga school ambacho kitasonwa na wengi na kitaishi kwa muda mrefu .
“Leo ni siku ya kuzindua rasmi chama hichi cha Tanga School Alumni Assoction lakini ifamike pia ndio siku ya kuzindua rasmi dhamira yetu ya kwenda kuanzisha maktaba ya kimtandao yaani library pale Tanga school ,hatua hii inalenga kuboresha miundombinu ya shule na kiwango cha ufaulu na ni chachu ya mageuzi makubwa ya kuinua viwango vya taaluma kulingana na kasi ya teknolojia ya sasa”allisema Semfuko.
Semfuko amewataka TSAA wote na wadau washikamane katika umoja huo kuhakikisha wanatekeleza kwa viwango vya juu na wanaweka utaratibu mzuri wa kulidumisha na kuboresha kizazi hata kizazi.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza