November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NBAA yazindua viwango vya maendeleo endelevu

Muhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi CPA Azizi Kifile akizungumza wakati wa uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu yenye lengo la kusaidia serikali katika juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu 2030 (SDG 2030) uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imezindua viwango  viwili vya utoaji taarifa  kimataifa vya kuripoti maendeleo na hatua endelevu kwa taasisi binafsi za serikali zikiwemo za taasisi za kifedha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi huo Muhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi CPA Aziz Kifile amesema viwango hivyo  vitasaidia kupanua wigo katika utoaji wa taarifa kwa taasisi za binafsi na serikali katika  kuelekezea umma hatua wanatakazochukua kuelekea mwaka 2030

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya taifa ya wahasibu na wakaguzi profesa CPA Sylivia Temu amesema lengo ni kusaidia serikali katika upatikanaji wa taarifa za fedha.

Viwango hivyo vya kuripoti IFRS ni vya wazi ili kuona dira ya maendeleo endelevu na athari katika mazingira vinatarajiwa kuanza kutumika kwa sekta zote ifikapo mwezi january2 024.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akziungumza kuhusu namna walivyojipanga kuweza kusimamia Viwango Vipya vya Hesabu vya kimataifa vya Kuripoti Maendeleo Endelevu na jinsi NBAA itakavyosaidia Taasisi mbalimbali katika kufikia malengo hasa kwenye kutumia viwango hivyo.

 

Mjumbe wa Bodi ya Kimataifa ya mahesabu kwa Sekta ya Umma (IPSASB), CPA Dkt Neema Kiure akiwasilisha mada kwa wadau mbalimbali waloudhuria uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu.

 

Mgeni Rasmi Muhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi CPA Azizi Kifile (kushoto) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Viwango Vipya vya Hesabu vya Kimataifa vya Maendeleo Endelevu yenye lengo la kusaidia serikali katika juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu 2030 (SDG 2030). Viwango hivyo ni Uwazi katika kuripoti maendeleo endelevu (IFRS S1) na Uwazi katika kuripoti athari za kwenye mazingira (IFRS S2) vitakavyotumiwa na Taasisi zote nchini Tanzania za Umma na Binafsi kuanzia Januari 01, 2024, Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius A. Maneno.

 

Mgeni Rasmi Muhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi CPA Azizi Kifile  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno, Wafanyakazi wa Bodi hiyo pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Viwango vya kimataifa vya Maendeleo Endelevu uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.