November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Mussa awataka wananchi Kata ya Mnyamani kutembea kifua mbele

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Diwani wa Kata Kiwalani Mussa Kafana, amewataka wananchi wa Kata ya Mnyamani Watembee Kifua mbele kwani vyama vya upinzani hawana uwezo wa kushika dola, vyama hivyo sawa na waosha mkaa.

Diwani Mussa Kafana, ameeleza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mnyamani Mji mpya wakati wa kuekezea utekelezaji wa Ilani kwa wananchi wafahamu kazi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

“Ninawaeleza wakazi wa Mnyamani amna chama chenye uwezo wa kushika dola kuanzia Serikali ya Mtaa, Udiwani na Ubunge sababu wao sawa na waosha mkaa pia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawana wawakirishi Bungeni “alisema Kafana.

Kafana alisema Serikali ya awamu ya sita inafanya mambo ya maendeleo kata ya Mnyamani Barabara zinajengwa huduma za kijamii pamoja na kuboresha miundombinu ni kazi inayofanywa katika usimamizi wa Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli na Diwani wake Shukuru Dege hivyo wawaunge mkono katika juhudi hizo kwa maendeleo ya Mnyamani.

Alisema CCM ndio chama kinachoshirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake hivvyo wananchi wasirubuniwe na vyama vya upinzani vya waosha mkaa ambavyo havijitambui ukitaka maendeleo baki ccm .

Diwani wa Kata ya Mnyamani Shukuru Dege alisema kata ya Mnyamani Serikali ya chama cha Mapinduzi CCM imefanya mambo makubwa kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, wamejenga shule ya kisasa ya Msingi, ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata kwa ajili ya kutoa huduma za Serikali pamoja na kituo cha afya cha Plan, kufanyiwa upanuzi kinaendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Diwani Shukuru Dege alisema shule ya Msingi Mnyamani mwaka 2024 itaanza kufundisha wanafunzi wa shule ya awali na shule ya Msingi ambapo wanafunzi wanaotarajia kuanza darasa la kwanza waliopokelewa mpaka sasa 200 na wa darasa la awali 100..

“Chama cha Mapinduzi CCM ni Baba lao maendeleo ya Mnyamani yanaenda kwa kwa kasi kubwa Miundombinu ya Barabara itakayojengwa mwaka huu Barabara ya Plan ,faru na Barabara ya mtaa Diwani zote zinajengwa kabla 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Mnyamani Mbaraka Mwinyimkuu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la segerea na Diwani wa Mnyamani wamefanikisha kujenga shule ya Msingi ya kisasa ,wamefanikisha kujenga ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata na sasa Barabara za ndani zinajengwa kwa kiwango cha lami yote hayo ni matunda ya ccm katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapunduzi CCM .

Mwenyekiti Mbaraka Mwinyimkuu aliwataka wananchi wajiunge na chama cha Mapinduzi kina fursa nyingi za uchumi na Maendeleo..

Mjumbe wa Kamati ya siasa Tawi la ccm Mji mpya kata ya Mnyamani Anuary Jumaa Mlugu alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi ccm vizuri na viongozi wake walioko madarakani .

Anuary Juma Mlugu alisema kwa mapenzi yake mwenyewe yeye anapenda juhudi za Serikali ndio anamuunga mkono Rais aliyepo madarakani kwa kusimamia miradi vizuri .