Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora
WADAU wa kilimo na wakulima kutoka Mikoa mbalimbali nchini walioshiriki Maonesho ya Siku ya Mbolea Duniani kuanzia Oktoba 11-13 Mkoani Tabora wameshuhudia ufanisi mkubwa wa mbolea ya keen mavuno kwenye kilimo cha mboga mboga na mazao mengine.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Chipukizi uliopo mjini hapa wamekiri kupata manufaa makubwa baada kutumia mbolea hiyo.
‘Tunamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu makampuni binafsi kuzalisha na kusambaza mbolea yenye viwango kwa wakulima’ amesema Mzee Kelembi Nuhu mkulima kutoka Sikonge.
Mkulima Moses Kusenha (54) mkazi wa Kijiji cha Songambele Mkoani Katavi amesema mbolea ya maji maji ya Keen mavuno imemsaidia kuongeza kipato baada ya kuitumia kwenye kilimo cha nyanya na kupata mavuno mengi tofauti na miaka mingine.
Afisa Kilimo kutoka wilayani Urambo Mkoani Tabora Julius Moses amekiri kuwa mbolea hiyo ni nzuri sana, kwa kuwa ina uwezo wa kukuza na kustawisha mazao haraka hivyo kumwezesha mkulima kuongeza uzalishaji na kupata fedha nyingi zaidi.
Afisa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Keen feeders Ltd, Kanda ya Ziwa, inayozalisha na kusambaza mbolea hiyo, Richard Munis amesema Kampuni hiyo imekuja kumaliza changamoto za wakulima.
Amebainisha kuwa kati ya aina 3 za mbolea zinazozalishwa na Kampuni hiyo (keen busta, keen mavuno na keen mavuno-gold) hii ya 3 imeleta neema kubwa kwa wakulima.
Amefafanua kuwa licha ya zote kuwa na uwezo wa kukuza na kuzalisha, hii ya 3 ina uwezo wa kustawisha na kuzuia mmea kupukutisha maua kutokana na upepo hadi utakapokomaa.
Munis ameongeza kuwa kutokana na ufanisi mzuri wa mbolea hiyo mwaka jana na mwaka huu wametwaa tuzo ya uzalishaji wa mbolea bora..
Mwish
More Stories
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM