Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wananchi wa Wilaya ya Magu wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji damu ili kusaidia uwepo wa damu ya kutosha na kuweza kusaidia maisha ya wagonjwa .
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Bi. Rachel Kassanda wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 24 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo aliongoza Wananchi katika zoezi la uchangiaji damu na kutoa misaada mbalimbali katika hospitali ya Wilaya ya Magu kama sehemu ya kumbukumbu ya kuyaenzi maono ya Mwalimu Nyerere.
” Nawaomba wananchi wa Magu wajitolee kuchangia damu ukiona afya yako ni nzuri na una uwezo njoo uchangie ili uokoe maisha ya mtanzania mwenzako mwenye uhitaji ambae angeweza kupoteza maisha kwa kukosa damu yako ” amesema DC Kassanda
Amesema Wilaya ya Magu imeadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa kwa kuwajulia hali wagonjwa na kutoa misaada mbalimbali katika hospitali ya Wilaya ya Magu kama ishara ya kuyaenzi maono ya Baba wa Taifa.
” Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mwakilishi wake Mkuu wa Wilaya ya Magu tumemkumbuka Baba wa Taifa kwa kuwatembelea wagonjwa na kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji waliopo katika wodi mbalimbali Hospitali hapa”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa waendesha bodaboda Wilaya ya Magu , Mohamed Jumanne amesema wameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Wilaya ya Magu kuadhimisha kumbukizi ya miaka 24 ya kifo cha Baba wa Taifa kwa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto na kusaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
Aidha Mwenyekiti huyo amewahamasisha vijana mbalimbali waliopo Wilaya ya Magu kuendelea kujitokeza kuchangia damu katika hopsitali zilizopo Wilaya ya Magu .
Matukio mbalimbali katika picha
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza