November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yapokea malalamiko ya Kodi kutoka AZAKI

Na Joyce Kasiki,Dodoma

SERIKALI  imepokea malalamiko  kutoka kwa Asasi za Kiraia na mashirika yasiokuwa ya Kiserikali (AZAKI)kuhusu suala la kodi wanazotozwa ilihali hawafanyi Biashara yoyote.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Hali ya Kikodi kwenye Asasi za Kiraia  leo Oktoba 3,2023 Jijini Dodoma, Kamishna wa Uchambuzi wa Sera na Utafiti Kutoka wizara ya fedha na Mipango William Mhoja  amesema Mamlaka ya Mapato itayafanyia Kazi Ili kujitidhisha na   hoja zilizoletwa na  AZAKI”

Amesema Kutokana na hilo watafanya vikao vya mara kwa mara ili kusudi pasiwepo na malimbikizi ya changamoto ambazo wao wanaziona kama zimejitokeza na mpaka sasa wamezichukua.

Kwa mujibu wa Mhoja, kwa zile Asasi zilizowasilisha maombi ya kutokuwasilisha Retani zao kwa wakati huku wakijua hawajafanya Biashara, wameomba msamaha kwenye maeneo hayo na suala hilo linahitaji maamuzi makubwa hivyo wameyachukua pia na wanaenda kuyafanyia Kazi Ili waone kama Kuna haja ya kutoa Tax Amnesty.

Kamishna huyo amesema wao kama Serikali wamejipanga kuimarisha mfumo wa Mapato Ili kuhakikisha wateja wanapata huduma ipasavyo na kwa wakati zaidi.

Naye  Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Bw.Onesmo Olengurumwa amesema kwa mwaka huu 2023 Asasi za Kiraia takribani Elfu 1000 zimeingiza Shiling Trilioni 2 hivyo ni sekta kubwa ambayo imekuwa ikisaidia Serikali katika kuendesha miradi mbalimbali nchini.

“Hii ni TASAF ya Wananchi kama Ilivyokuwa kwenye upande wa Serikali, maana hii Wananchi kupitia Asasi zao wameona Kuna Changamoto ya kijamii  wametengeneza  taasisi zao, wanatafuta wahisani kwa Ajili ya kutatua hizo Changamoto” Amesema.

Olengurumwa amesema wao kama sekta isiyojipatia Faida wana umuhimu wa kukaa na Serikali kurekebisha Sheria zao Ili waweze kwenda sawa katika kila kitu.