November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CPB yataka wananchi waitumie Bodi kupata chakula Bora

Na David John timesmajira oniline Geita

AFISA Mauzo na usambazaji kutoka Bodi ya Nafaka na  Mazao Mchanganyiko Kanda ya ziwa Francisco Amos amesema kuwa i maonyesho ya madini mkoani Geita yamekuwa yamafanikio makubwa kwao kutokana na wananchi wengi kutembelea Banda lao na kununua bidhaa zao.

Amos ameyasema hayo septemba 30 mwaka huu katika hitimisho la maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini ambayo yanafanyika Kila mwaka mkoani humo .

Amos Amesema licha ya kwamba ni mara yao ya kwanza kushiriki kwenye maonyesho hayo lakini yamewapa picha nzuri kwamba wakati mwingine waje vizuri zaidi  nakwamba  wananchi wamependa bidhaa na huduma na wameonyesha uhitaji mkubwa zaidi.

“Kwakifupi naweza kusema maonyesho yamekuwa tofauti na tulivyotarajia kwani tulikuja kama kuona kama bidhaa watazipenda lakini kimsingi majibu yamekuwa mazuri na wametembelea wengi na bidhaa zimechukuliwa za kutosha na tumepata mawakala wa kutosha na wasambazaji wengine wakutosha.”Amesema Amos

Amesema kuwa meseji kubwa ambayo inapelekwa Kwa wanageita na Kanda ya ziwa ni kwamba hasa wakulima na wadau wote ambao wanahusika katika sekta ya nafaka na kilimo Kwa ujumla ni  Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko imetengenezwa maalumu au kuundwa maalumu Kwaajili ya kuja kuwa Jukwaa litakalokuja kuwanufaisha  wakulima .

Ameongeza kuwa anatoa wito Kwa wakulima waendelee kulima mazao yao kisasa waendelee kuboresha mashamba yao na vitu mbalimbali vinavyotimika kwenye kilimo ili waendelee kupata mazao ya kutosha kwani Soko la bidhaa zao lipo na Bodi ya nafaka ni Jukwaa muhimu sana na lina maana sana ambapo wao wanaweza kuuza mazao yao hivyo wanageita na watanzania waendelee kulima na baada ya hapo bidhaa zao zipo kwenye supermarket na maduka mengine zitapatikana na Kwa Bei nafuu kabisa .

“Uhakika wa bidhaa upo na wakati mwingine tutakuja vizuri zaidi na bidhaa nyingi ambazo wananchi wameziulizia  na kuhusu changamoto wananchi wengi wanakosa elimu ya kutosha hasa inapofika suala la ubora wa chakula na wanamitazano furani kuhusu ubora wa chakula hivyo  wakati mwingine tutakuja vizuri zaidi na kuwaeleza wananchi kuhusu ubora wa chakula lakini pia kuwajengea uwezo wa uelewa zaidi .