Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
SERIKALI imewataka Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini kuhakikisha wanafanya kazi kwa misingi ya uadilifu na uaminifu wa hali ya juu ili kuongeza tija na ufanisi katika maendeleo ya nchi.
Akizungumza kwenye mahafali ya 45 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Elijah Mwandumbya amesema NBAA inatakiwa kuisaidia serikali na kuhakikisha kanuni na miongozo ya uadilifu inafuatwa na wanachama wake wote ili atakaenda kinyume hatua kali zichukuliwe dhidi yake na iwe fundisho kwa wengine.
Mwandumbya amesema halmashauri zote nchini ziwatumie wataalamu wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ili kupunguza migogoro ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inawakabili wananchi katika kutekeleza miradi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu amewataka wahitimu wote kuhakikisha wanasoma taratibu za NBAA ili waweza kujua ni namna gani ya kwenda kufungua ferm ya mahesabu na sio kwenda kusaini mahesabu.
Hivyo, ametoa rai kwa wazazi, walenzi na wajaajiri wa Sekta za umma na binafsi kuendelea kuwasapoti vijana na watumishi wao ili waweze kufanya mitihani ya bodi na kufuzu kwa uwekezaji wa taaluma ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ni uwekezaji unaolipa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Elijah Mwandumbya akisoma hotuba yake kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye mahafali ya 45 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo katika hoteli ya APC Bunju mkoani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu akizungumza kuhusu namna Bodi hiyo ilivyofanikisha kutoa wahitimu pamoja na mafanikio ya Bodi hiyo wakati wa mahafali ya 45 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo katika hoteli ya APC Bunju mkoani Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akitoa ufafanuzi kuhusu Bodi hiyo inavyofanya kazi zake kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Elijah Mwandumbya aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na wahitimu wa Bodi hiyo wakati wa mahafali ya 45 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Elijah Mwandumbya aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba akitoa vyeti kwa baadhi ya wahitimu waliofanya vizuri kwenye mitihani ya Bodi wakati wa mahafali ya 45 ya Bodi hiyo yaliyofanyika leo katika hoteli ya APC Bunju, Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahitimu pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Elijah Mwandumbya aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye mahafali ya 45 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) yaliyofanyika leo katika hoteli ya APC Bunju mkoani Dar es Salaam.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa