November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TCAA yasaini mkataba wa Bil. 9/-


Na Jackline Martin, TimesMajira Online


MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA) imetia saini mkataba na Kampuni
ya Indra Avitech GmbH wenye thamani ya
sh. bilioni 9 kwa ajili ya kubuni, kusambaza,
kusanikisha, kuunganisha na kuzindua mfumo wa usimamizi wa Taarifa za Anga (AIM).


Lengo la utekelezaji wa mradi wa mfumo huo ni kuboresha mfumo wa AIM katika kuboresha usahihi wa data, upatikanaji na ufanisi kwa kuzingatia mahitaji ya upandishaji wa mfumo wa Anga wa Usafiri (ASBU) na kufuata viwango vya kitaifa na Kimataifa.


Akizungumza na waandishi wa habari
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa utiaji Saini mkataba, Mkurugenzi Mkuu Wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TCAA), Hamza Johari, alisema mradi huo utatekelezwa kwa miezi 18 na utaanza mara tu baada ya kusainiwa kwa mkataba.


Alisema Tanzania inakuwa nchi ya tano
Afrika kufunga mfumo huo ikiwa ni baada ya nchi ya Kenya, Uganda, Eswatini na Ghana.


“Hii ni sehemu ya mpango thabiti wa AIM
wa kuboresha mfumo wake wa taarifa za Anga kwa kutoa usimamizi wa taarifa za Anga kwa njia ya kisasa zaidi kwa kutoa na kubadilishana taarifa za Anga za kidigitali zenye ubora na kushirikiana na pande zote hivyo kuhakikisha usalama, utaratibu na ufanisi wa usambazaji wa anga wa kitaifa na kimataifa”


Aidha alisema kwa sasa TCAA imekuwa
ikisimamia taarifa za Anga kwa njia ya kawaida, NoTAMs kutengeneza nyaraka muhimu za AIM kama mchapishaji wa taarifa za Anga na kutoa huduma za Mipango ya safari na utambuzi wa
awali wa safari, hivyo kuimarisha michakato hiyo kwa njia ya kiotomatiki kutaimarisha uzingatiaji wa TCAA kwa viwango na taratibu zinazopendekezwa na Shirika la Usafiri wa Anga la Kimataifa na kuleta manufaa kwa wadau kwa kuboresha utoaji wa huduma za
AIM.


“Wadau wa TCCA wanapaswa kutarajia
upatikanaji wa wakati unaofaa wa taarifa za Anga zenye ubora wa hali ya juu kwa muundo wa digitali, Mipango ya safari yenye ufanisi na huduma za utambuzi kupitia mfumo wa Mipango ya safari kwenye wavuti.


Makampuni ya ndege na watoa huduma
za Anga wataweza kutekeleza huduma za
utambuzi kabla ya safari katika eneo lao,
watakuwa na upatikanaji wa taarifa zote
muhimu kama NoTAMs, taarifa za hali ya hewa na taarifa za mchapishaji wa Taarifa za Anga wa elektroniki mtandaoni ili kupanga safari zao kwa ufanisi” Alisema Mkurugenzi Johari


Alisema watoa taarifa za Data wa TCAA
wanapaswa kutarajia kuboresha njia
wanayosambaza taarifa muhimu kwa idhini ya TCAA, kwani tovuti ya kutoa Data itaruhusu watengenezaji wa Data za Anga kuwasilisha taarifa muhimu kwa TCAA badala ya kutumia mchakato wa kawaida wa kibinafsi. Meneja Miradi na Mauzo kutoka kampuni ya Indra Avitech, Simon Masike alisema programu hiyo itawezesha data za anga kuhifadhiwa na kuhamishiwa kwenye programu maalumu kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za anga kwa njia
ya kiotomatiki.


“Tunafurahi kuwa sehemu ya kutekeleza
mradi huu ambao utakuwa na mchango
mkubwa katika kuboresha usalama wa safariza angani kutokana na kutoa taarifa zenye ubora,” alisema Masike.
Samia