Na Moses Ng’wat,Timesmajiraonline,Songwe
WAFANYABIASHARA katika soko Kuu la Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe, wamesitisha mgomo wao wa kufunga maduka yao zaidi ya 400 uliodumu kwa siku moja baada ya kukubali maombi ya serikali ya Mkoa ya kuwataka wafungue na kuendelea kutoa huduma wakati malalamiko yao yakishughulikiwa.
Wafanyabiashara hao walilazimika kufunga maduka yao wakilalamikia ongezeko kubwa la kodi ya pango, pamoja na uchakavu wa baadhi ya miundombinu katika soko hilo.
Mwenyekiti wa soko hilo, Aron Mkea, kizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 22, 2023, amesema wafanyabiashara wameamua kufungua maduka yao mara baada ya kukutana na Mkuu wa Mkoa .
“Kwa kuwa suala la utatuzi ni mchakato na tayari Mkuu wa Mkoa ameagiza suala hili liishe, wafanyabiashara wamekuhali wafungue biashara zao wakati Halmaahauri inafanyia kazi malalamiko yetu,
” Katika kikao kile na Mkuu wa Mkoa ameagiza kuwa Halmashauri zisimamishe tozo zote zinazohusiana na mkataba wa upangaji na zichakatwe upya,”amefafanua Mwenyekiti Mkea.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Soko la Tunduma ni kwamba Halmashauri ya Mji Tunduma ilipandisha kodi ya pango bila kuwashirikisha wafanyabiashara kutoka shilingi 50,000 kwa vibanda vya ndani na 70,000 hadi kufikia shilingi 100,000 kwa vibanda vya nje na shilingi 70,000 kwa vibanda vya ndani.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Belton Garigo ambaye ni Mkuu wa divisheni ya Mipango na Uratibu amesema Halmashauri hiyo ilipandisha kodi ya pango katika soko hilo mwaka 2021 baada ya kumaliza kwa mkataba wa ujenzi kati ya wafanyabiashara hao na Halmashauri.
“Mwanzo wafanyabiashara walikuwa wakilipa Kodi ndogo ili kudia gharama za ujenzi, lakini baada ya muda kuisha na vibanda hivyo kurudi mikononi mwa Halmashauri ilipanndisha kodi kulingana na hali ya soko,”amefafanua Kaimu Mkurugenzi Gargo.
Akizungumzia kuhusu maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa katika kikao chake na wafanyabiashara, Gargo kimsingi Halmasuri imeanza mchakato wa kushughulikia maagizo yote.
Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk. Francis Michael, ameagiza Halmashauri hiyo katika kipindi cha kuanzia sasa hadi Disemba mwaka huu, kusitisha ukusanyaji wa kodi ya pango kwa mujibu wa mkataba mpya wa mwaka wa fedha 2023/ 24.
Maelekezo mengine yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ni Halmashauri hiyo ndani ya kipindi hicho cha miezi mitatu wawe wamerekebisha njia ndani ya soko hilo, kukarabatiwa kwa choo, pamoja na kukarabati eneo la paa.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa