Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkurugenzi Mtendaji wa LG Electronics Afrika Mashariki, Dong Won Lee amesema kutokana na Dar es Salaam na Dodoma kukua kwa kasi kubwa, wataendelea kuleta mabadiliko katika biashara ya joto, hewa safi na viyoyozi yaani Heating, Ventilation and Air Conditioning (HVAC) ambavyo kila mtanzania anapaswa kuchangamkia.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa sasa kutakua na mabadiliko makubwa katika mfumo wa viyoyozi kutoka kwakampuni ya LG electronics ambayo imeleta sokoni viyoyozi vipya na vya teknolojia ya hali ya juu.
Mkurugenzi huyo aliyasema hayo aliyasema wakati akizungumza katika Hafla ya wahandisi ambayo hufanyika Kila mwezi wa tisa yenye lengo la kuleta pamoja wahandisi, wazalishaji na taasisi za kiserikali kuonesha ubunifu wa aina mbalimbali ikiwemo teknolojia ya HVAC ambapo zaidi ya wadau 4000 walihudhuria hafla hiyo mwaka huu.
“Viyoyozi hivyo vimeoneshwa kwa mara ya kwanza katika maonesho maalumu ya siku mbili yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi maarufu kama Milimani Exhibition Center Jijini Dar es Salaam, Tanzania.”
“Ushiriki wetu katika maonesho hayo ni kudhihirisha nia ya kuwapa kuwawezesha watanzania kupata huduma bora ya viyoyozi kwa kutumia umeme mdogo.”
Dong Won Lee amesema HVAC ya LG imelenga kutoa huduma inayozingatia afya za watumiaji, mazingira bora ya makazi na sehemu za kazi kwani kampuni hiyo inatumia teknolojia ya kisasa ambayo inaendana na malengo ya dunia nzima kupunguza uchafuzi unaosababishwa na gesi ya carbon kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.
“Kama kiongozi katika soko hili, LG itaendelea kuendeleza teknolojia ya HVAC na kuja na suluhisho bora ya kuhakikisa hewa safi na ndani kwa wateja wote kutoka Tanzania,” amesema Dong Won Lee,
Aidha Don Wee Lee amesema kuwa vifaa hivyo ni vya umuhimu kwani kwa sasa kuna ujenzi mwingi unaondelea Jijini Dodoma ikiwemo ujenzi wa nyumba 250 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutokana na ongezeko za shughuli za Serikali Jijini hapo.
Aidha alisema Jijini Dar es Salaam kuna ongezeko kubwa la uhitaji wa maofisi, hoteli na sehemu za biashara yote haya yakisababisha ujenzi wa majengo mbalimbali yakiwemo magorofa marefu ambayo yanahitaji teknolojia ya hali ya juu ya viyoyozi, jambo ambalo LG imejipanga kushugulikia.
Katika maonyesho hayo LG imeonesha viyoyozi vya aina mbalimbali ikiwemo Dual Cool Inverter Wall split za majumbani, Smart Inverter, viyoyozi vya Split, feni za juu na friji na Smart Inverter Compressor.
” Moja ya teknolojia za hali ya juu zilioneshwa kupitia mashine ya Single Split Commercial Air Conditioner (SCAC), ambayo inapunguza matumizi ya umeme kwa asilimia 40 kutokana na compressor yake kuwa na uwezo wa kubadilisha spidi ili kupata ubaridi unaotakiwa. SCAC sasa inapatikana kwa mfumo wa viyoyozi vya kusimama na ina spidi ya upozaji ya asilimia 30. “
Teknolojia nyingine zilikuwa pamoja na Multi V5 ambazo zinatumika kwenye majengo ambayo ni teknolojia ya hali ya juu inayohakikisha ufanisi wa hali ya juu kwa umeme mdogo.
More Stories
RC Mtambi awataka Maofisa kilimo kutoa elimu ya kilimo mseto
Rais Samia kuelekea nchini Brazil kushiriki mkutano wa G20
Rais Samia atoa maagizo ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo