November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakuu wa nchi Afrika wajadili mikakati mbalimbali kukabiliana na mifumo ya chakula Afrika,Wajumbe zaidi 5000 Afrika walishiriki mkutano

 Na David John timesmajira online 

MNAMO  Septemba 8, 2023, viongozi wa Afrika walikusanyika jijini  Dar es Salaam Tanzania kwa ajili ya Mkutano wa Kilele wa Rais kama sehemu ya Kongamano la Mifumo ya Chakula Afrika 2023. 

Jukwaa ambalo linakamilika Leo septemba 8 ,2023 lilichukua zaidi ya wajumbe 5000 kutoka kote ulimwenguni kuchunguza sera, mafanikio na ubunifu ambao utaharakisha mabadiliko ya mifumo ya chakula barani Afrika.

Wakati wa mkutano huo, Wakuu wa Nchi kutoka Tanzania, Kenya, Burundi, Senegal na Zanzibar walijadili hatua mbalimbali ambazo nchi zao zinatekeleza ili kubadilisha mifumo yao ya chakula kwa lengo la kukabiliana na uhaba wa chakula na kuimarisha ustahimilivu.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa kongamano la mkutano huo wa Jukwaa la Mifumo ya chakula Afrika . Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisisitiza dhamira ya nchi yake ya kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo na kuibuka kuwa mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika.

“Ninaamini kuwa Afrika inaweza kulisha dunia na serikali yangu imeongeza bajeti ya kilimo karibu mara nne, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kutoka dola za Marekani milioni 120 mwaka 2021/2022 hadi dola milioni 400 mwaka 2023/24 katika jitihada za kuchochea kilimo na mageuzi ya mfumo wa chakula nchini Tanzania,” alisema.Rais Hassan

 Pia aliwataka viongozi wa Afrika kuendana na Azimio la Malabo ambalo linayaamuru mataifa ya Afrika kutenga kima cha chini cha asilimia 10 ya bajeti zao kwa kilimo, ikilenga angalau asilimia sita kwa kiwango cha ukuaji wa kila mwaka.

Akizungumza katika hafla hiyo, H.E. hailemariam Dessalegn, Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Kikundi cha Washirika wa AGRF aliangazia maswala muhimu yanayokabili Mifumo ya Chakula ya Afrika ikiwa ni pamoja na mzozo unaoendelea wa Urusi na Ukraine, athari mbaya za janga la COVID-19, kuongezeka kwa ukame na mafuriko, usumbufu wa usambazaji,migogoro, na masuala mengine muhimu

“Tuko katika harakati za kupona kutokana na mishtuko mitatu mikuu na hitaji la kuchukua hatua za kuleta mabadiliko halijawahi kuwa la dharura zaidi. 

Jukwaa la Mifumo ya Chakula barani Afrika 2023 ni wakati mahususi wa kuangazia na kufungua ahadi za bara hili za kisiasa, kisera na kifedha na ubunifu kuelekea kufikia mifumo yenye tija, yenye lishe, shirikishi, thabiti na endelevu ya chakula barani Afrika,” alisema.

kikao kilishirikisha wahudhuriaji wengine mashuhuri akiwemo H.E. Lionel Zinsou, Waziri Mkuu wa Zamani, wa Jamhuri ya Benin; H.E. Dkt Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jonathan Goodluck, Rais wa zamani wa Nigeria na H.E. mohamed Beavogui, Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea.