December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Nyasika aeleza mikakati ya maendeleo

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

DIWANI wa Kata ya Kivule (CCM)Nyasika Getama, ameeleza mikakati yake ya Maendeleo ndani ya kata ya Kivule kwa kushirikiana na Wananchi wake .

Diwani Nyasika Getama ,amesema mikakati ya kwanza waliopanga na Wananchi wake kipaumbele ujenzi wa kituo cha kisasa cha Polisi ambapo kila Mwananchi atachangia shilingi matofali mawili Diwani wa Kata hiyo Nyasika yeye amechangia shilingi 500,000/= ya matofali .

“Kata ya Kivule itajengwa na wananchi wa Kivule wenyewe tumeweka vipaumbele mwaka huu tutajenga kituo cha Polisi kwa nguvu ya Wananchi ameomba Wananchi washiriiane katika mkakati kuleta Maendeleo “amesema Nyasika

Diwani Nyasika amesema dhumuni la kujenga kituo hicho cha Polisi kuimalisha ulinzi na usalama ambapo Serikali imefanya mambo makubwa Kivule Ina miradi ya Serikali mikubwa vituo vya afya Hospitali ya Wilaya lakini aina kituo cha Polisi chenye askari wa kutosha .

Akizungumzia sekta ya elimu alisema katika Uongozi wake amefanikiwa kujenga vyumba 20 vya Madarasa ya sekondari na mikakati iliyopo Kivule kuwa na shule ya Wasichana Pekee ijengwe na mabweni dhumuni Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.$amia Suluhu Hassan ataki watoto waende shule za Mbali kusoma ,awali kulikuwa na shule ya Sekondari ya Misitu ambayo imeongezwa madarasa manne na Serikali .

Aidha alisema shule za msingi mwanzo zilikuwepo nne lakini kutokana na ukubwa wa Kata hiyo shule za msingi zipo sita zote zimejengwa kwa mapato ya ndani .

Akizungumzia Miundombinu ya Barabara za ndani alisema barabara ya Kivule Msongola itajengwa April 2024 hivyo amewataka Wananchi kuwa watulivu Serikali ina mipango mizuri ya Maendeleo ndani ya kata hiyo itakuwa ya kisasa hivi karibuni .

Aliwataka Wananchi kulipa kodi ya Serikali ili kuongeza mapato ya hamashauri ya Jiji hilo ambalo linafanya vizuri katika sekta zote mara baada kuigawa Ilala Kanda Saba za utoaji huduma na ukusanyaji mapato .

Katika hatua nyingine aliwataka Wananchi wa Kivule kwenda na mabadiriko kuwa na namba za Serikali kila nyumba (posti Kodi)wale ambao bado waatalam watafika Kata na kuwashirikisha Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Ili Namba ziwekwe waweze kutambulika mitaa yao pamoja na nyumba katika mfumo .