Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
WALIMU nchini wametakiwa kujiondoa kwenye ‘mikopo umiza’ inayowadharirisha kama watumishi muhimu sana kwenye taifa na badala yake wametakiwa kujiunga na Mwalimu Commercial Bank (MCB) benki ambayo ni yao.
Mwanahisa wa MCB Mwalimu Romana Kimambo kutoka wilaya ya Kisarawe, Coast Region, aliyasema hayo katika majadiliano yaliyowakutanisha wanahisa wa benki hiyo jana jijini Dodoma katika mkutano wao was aba tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.
Wanahisa, wayasema haya kwa uchungu mkubwa sana, tumefanyakazi nzuri ya kutafuta mitaji na hatimaye kuanzisha Benki ya Biashara ya Mwalimu (MCB), lakini cha kushangaza baadhi ya walimu wenzetu wanachelewa kujiunga huku wakiendelea kuhangaishwa na kuhangaika na mikopo umiza maarufu kama kausha damu.
Jambo hili linaniumiza sana, nina wahurumia walimu wenzangu, natoa rai wajitoe huko walikokamatika, waje MCB iwape matumaini yao wanayoyatamani, alisema Romana kwa uchungu mkubwa.
Mwanahisa mwingine, Mwalimu Eliud Ole Mtambala, wa shule ya Msingi Chamwino, Kata ya Chamwino Halmashauri ya Jiji la Dodoma, pamoja na uchanga wa benki yao lakini yeye tayari ameanza kula na kufaidi matunda ya mkopo ambao hauna kusumbuana.
Akaendelea kusema, wako baadhi ya walimu wenzetu wameingia kwenye mikop ya ajabu ajabu na wamelazimika kukabidhi hadi kadi zao za kibenk kwa wakopeshaji, ili mishahara inapoingia tu, mkopeshaji aweze kutoa fedha yake na kinachosalia kinaelekezwa kwa Mwalimu, lakini kinachoumiza zaidi ni kwamba mikopo hii ya ajabu ina riba kubwa ambayo ni vigumu kumkwamua Mwalimu na kumwacha katika nafasi ya kuweza kujenga taifa la kesho.
Akifungua mkutano huo uliojaa wanahisa kutoka kila upande wa nchi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Francis Ramadhani, aliwahakikishia wanahisa wote wa Mwalimu Commercial Bank (PLC), kuwa benki hiyo inaendelea kukua kufuatia mageuzi yanayoendelea yaliyoanzishwa tangu mwaka 2019.
“Nataka kuwahakikishia wanahisa wotey, mageuzi makubwa yanayoendelea kufanywa ndani ya benki yetu, ni ya msingi na yamesaidia kuiinua MCB hatua kwa hatua hadi mwaka 2022,”. Amesisitiza Mwenyekiti Francis.
Akasema, ili Mwalimu Commercial Bank (MCB) iweze kufanya vizuri zaidi ni lazima wafanyakazi waendelee kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika kuwahudumia wateja na, hii ndiyo itakuwa tofauti kubwa kati ya MCB na benki nyingine nchini ambapo ushindani wa sekta ya fedha umeendelea kukua kila iitwapo leo.
“Tumefikisha miaka saba mwaka 2022 katika utoaji wa huduma tangu benki ianzishwe, na katika kipindi hicho benki imeweza kukuza mali na thamani yake kwa zaidi ya mara mbili yaani kutoka kuwa na kiasi cha 30 bilioni hadi kufikia 83 bilioni,” Amesema Francis.
Wakati kitabu cha mikopo cha MCB kikikua mara nne zaidi kutoka shilingi 16 bilioni na kufikia 64 bilioni, imebainika kuwa amana za za wateja nazo zikiongezeka kutoka thamani ya shilingi 11 bilioni hadi kufikia 60 bilioni.
Kadhalika kwa mujibu wa Mwenyekiti Francis, mapato ya MCB yameongezeka kutoka 2.8 bilioni hadi kufikia 7.2 bilioni Tanzania Shillings, hiki kinaonekana kama kiashiria kikubwa cha ufanisi na ukuaji wa MCB.
Haya ni maendeleo makubwa katika ukuaji wa benki yetu na hakika tuna kila sababu ya kujivunia, hatua hii ambayo tumeifikia, nasi kwa pamoja baina ya bodi na menajiment, tunaamini kuwa Mwalimu Commercial Bank itaendelea kuwa imara na kuendeleza kasi hii ya kufanya biashara ili kuleta thamani ya uwekezaji wa wanahisa wetu hadi kufikia hatua ya kutoa gawio kwa wanahisa wetu.
Katika mpango wake wa kujipanua MCB kufikia Desemba 2022, ilikuwa na matawi mawili jijini Dar es Salaam, pia imefungua ofisi nane za kanda katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kigoma, Rukwa, na Mtwara ili kuwafikia wadau kwa urahisi katika hatua hii uchanga wake.
Pamoja na kufungua ofisi za kanda, MCB pia imewafifika wajeta wake kwa njia rahisi za kiganjani,, mobile App, pia kwa kutumia Mwalimu Card Visa kwenye ATM zake zaidi ya 1500 nchi nzima sambamba na mawakala wake wanaofikia 474.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa muundo wa umiliki wa wanahisi ni ule wa Mwalimu Mwalimu mmoja mmoja ambao ndiyo waanzilishi wa benki pamoja na taasisi zao ambazo ni Chama Cha walimu Tanzania na TDCL, kwa pamoja wanamiliki hisa asilimia 51.4 ya his azote, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSSF) na umma kwa ujumla wanamiliki asilimia 16.2 kila mmoja.
Kulingana na taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania, sekta ya benki nchini imeendelea kuwa himilivu 4katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ni pamoja na ukwasi na upungufu wa mitaji ya kutosha kwa benki nyingi.
Ambapo sekta ya mikopo kwa wateja imeendelea kukua kwa asilimia 22.5 na kwa upande mwingine amana za wateja zikiongezeka, hii ni ishara ya uchumi kuendelea kuimarika.
Tuna matarajio kuwa benki itaendelea kufanya vizuri mwaka 2023, ambapo katika nusu ya kwanza ya mwaka huu hadi kufikia June 30, 2023 tayari MCB ilikuwa imepata faida ya kiasi cha shilling 172 milioni baada ya makato ya kodi, na ni imani ya bodi na manejiment kuwa mwanzo huu mzuri hautaishia njiani, bali ni mbele kwa mbele, amesisitiza Mwenyekiti Francis.
Mkutano huo wa wanahisa pamoja na mambo mengine umejadili na kuidhinisha ripoti ya mwaka uliopita, na kujadiliana mipango ya kuendelea kuiimarisha MCB.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda