November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TTCL kujidhatiti kuboresha mkongo wa Taifa

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limejidhatiti kuendelea kuboresha Mkongo wa Taifa kufikia Terabyte 2 ifikapo Januari 2024, hali itakayowezesha kusogeza huduma za internet yenye kasi zaidi na kwa gharama nafuu kwa wananchi na
hivyo kuchochea uchumi wa kidigitali.


Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga, alisema shirika hilo kwa sasa limefikia wilaya 100 na lengo ni kuhakikisha wilaya zote nchini zinafikiwa ifikapo december 2024.


Vilevile alibainisha kuwa shirika hilo limedhamiria kuongeza ushirikiano na wizara ya fedha ili Kuwezesha malipo kwa njia ya mtandao hali itakayosaidia
kuongeza usalama wa fedha na vilevile kupunguza ubadhilifu wa fedha nchini.


“TTCL inaendesha mkongo wa Taifa na inatoa huduma za faiba mlangoni ambazo zitahakikisha wananchi wote wanapata mtandao wenye spidi kubwa nchi nzima”


Alisema wananchi mnapoona maendeleo
makubwa ya kimawasiliano nchini , wao ndiyo wapo katika kitovu na ndiyo mhimili mkuu wa mawasiliano ni TTCL .


Aidha alizitaja changamoto ambapo TTCL
wanakumbana nazo ikiwemo miundombinu kutokuwa wezeshi ambapo hadi sasa kazi kubwa inafanyika kuongeza upatikanaji wa miundombinu ya mawasiliano nchi nzima.


“Tulikua tunakumbana na changamoto kwenye Wilaya kam Mafia ambayo ilikuwa baharini, tumeshapata njia ya kuhakikisha kwamba tunaweza kufika katika kipindi kijacho cha mienzi takribani mitano”


“Sisi kama TTCL tunalibeba hilo na tunawawezesha wenzentu na Makampuni yote biinafsi waweze kutumia miundombinu hiyo, kujenga hiyo miundombinu inahitaji gharama, inahitaji nguvu kazi na kazi hiyo tumeshaanza kuifanya na ndiyo maana miaka ya
mwanzo inachukua muda mrefu na tunaamini miundombinu ikikamilka uchumi wa kidigitali utafika pale panapotakiwa.