November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Chalamila azindua Dhamana ya bidhaa ya kampuni ya ALAF

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amezindua dhamana ya bidhaa ya kampuni ya ALAF Tanzania, ambayo ni moja ya makampuni chini ya Safal Group, lengo likiwa ni kulinda ubora wa bidhaa zake kwa wateja katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo uliofanyika Jana Jijini Dar es Salaam, unatokana na kutapakaa kwa bidhaa zilizozalishwa chini ya kiwango pia bidhaa bandia katika soko la Tanzania na masoko ya nje.

Meneja Masoko wa ALAF, Isamba Kasaka alisema dhamana hiyo mpya,inalenga kuwapa walaji amani na kuwahakikishia kuhusu bidhaa za ALAF ambazo ni pamoja na mabati na nondo, ambapo amesema ALAF imeendelea kushtushwa na wimbi la bidhaa za chini ya kiwango na bidhaa bandia ambazo zinaathiri sekta zote nchini.

“Bidhaa hizi pia ni hatari kwa usalama na afa ya walaji,”.

Hata hivyo kupitia program hii ya dhamana ya bidhaa wataendelea kutoa elimu kuhusu bidhaa za chini ya kiwango na feki. “Tunafanya kazi kwa karibu na serikali, vyombo vya kuimarisha sheria na vyombo vya uthibiti ili kukabiliana na wimbi hili la bidhaa feki,” alisema.

Aidha RC Albert Chalamila, alipongeza kampuni ya ALAF kwa kuibua mjadala huu wa bidhaa bandia. Alitoa wito kwa vyombo vyote vya usimamizi na wadau wengine wote kuimarisha vita dhidi ya wimbi hili.

Alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kama vile TBS, FCC, OSHA na nyinginezo kuhakikisha wazalishaji wanazingatia ubora ili kuwalinda walaji.

“Walaji wanatakiwa kuichangamkia dhamana hii ya bidhaa ili wajirishishe na ubora wa bidhaa na uhalali wake kabla ya kununua,” amwsema na kusiistiza kuwa serikali itaendelea kusimamia kwa karibu suala la ubora.

Kwa mujibu wa Chalamila, ukosefu wa ubora una athari kubwa za kiafya, usalama kwa walaji na usalama wa Taifa hivyo unatakiwa kulindwa kwa nguvu zote.