November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali, Wadau kuja na mpango kudhibiti Magonjwa ya mlipuko, kuambukiza

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM

SERIKALI yashirikiana na wadau mbalimbali katika kufanya tathimin ya utayari wa kupambana na magonjwa ya mlipuko na kuambukiza ili kuhakikisha wanapata mpango mkakati wa utekelezaji ambao utawezesha kulinda afya za wananchi.

Akizungumza wakati washa hiyo Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi msaidizi sehemu ya ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa – Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya Vida Mbaga amesema lengo ni kufanya zoezi la kujipima utayari wa nchi katika kudhibiti majanga na magonjwa ya mlipuko yanayosababisha watu kuugua na vifo.

Aidha, Wizara ya Afya chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu inashirikiana na vyuo, taasisi na sekta mbalimbali katika kudhibiti magonjwa na majanga mengi, “leo tupo hapa na wadau kutoka nje ya nchi linakuwa ni zoezi shirikishi la kujipima kwa pamoja ili kuangalia mapungufu na kutengeneza mpango wa kudhibiti Magonjwa ya mlipuko, majanga mengi yanayoadhiri afya” amesema Mbaga

Naye Gerard Manase Afisa Afya (Kitengo Cha Udhibiti Magonjwa ya Mlipuko na Dharura za kiafya kutoka Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe – TAMISEMI ) amesema baada ya kukamilika mpango mkakati wa kudhibiti ndipo Ofisi ya Rais Ya Tamisemi itachukua hatua ya utekelezaji.

kwa upande wake Faraja Msemwa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Ofisi ya Tanzania amesema lengo la kufanya tathimin hii ni kutambua nafasi ambayo nchi ya Tanzania imefika katika uwezo wake wa kukabiliana na matokeo ya dharura.