Na Esther Macha,Timesmajira,Online,Mbeya
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa dhamira yake na kiu ni kuhakikisha kuwa anaendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kila wilaya ili waweze kujiinua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujasiliamali.
Amesema kuwa toka achaguliwe kuwa Mbunge wa kuwaongoza wanawake wa mkoa mbeya tangu achaguliwe kuwaongoza wanawake wa Mkoa wa Mbeya pia amewataka kuwa na mshikamano na umoja ndani ya jumuiya ya wanawake.
Mha. Mahundi amesema hayo leo wakati akitoa taarifa ya utekelezelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya mwaka 2020/2025 katika kikao mbele ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Dkt.Stephen Mwakajumilo katika ukumbi wa shule ya sekondari Mbeya ambapo amesema mshikamano na umoja vitawafanya wanawake kuwa pamoja na kusonga mbele.
Katika hatua nyingine Mhandisi Maryprisca Mahundi amewawezesha wanawake majiko ya gesi zaidi ya mia nane lengo ni kupambana na ukataji wa miti hovyo sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais.
Aidha Mahundi amesema kwa kushirikiana na wanawake atahamasisha wanawake kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za Rais ambapo amebuni kitenge ambacho kimewafikia wanawake zaidi ya elfu moja mia tano kilichogharimu zaidi ya shilingi milioni hamsini ambacho anakigawa bure.
“Hivi sasa wilaya zote za Mkoa wa Mbeya zinawezeshwa shilingi milioni ishirini kila Wilaya ili kujiimarisha kiuchumi kwa kujenga vitega uchumi na awali wanawake waliwezeshwa mitaji na sasa tarajio ni kuwawezesha mama lishe katika tamasha maalum litakalojulikana kama “Mama Ntilie Festival”ambapo watanufaika kwa kupatiwa mitaji na majiko ya gesi,”amesema.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Lupa wilaya Chunya ,Masache Kasaka alimshukuru Rais Dkt.Samia kwa kupeleka maji katika jimbo hilo ambapo katika jimbo hilo kulikuwa na changamoto ya upatikanaji maji .
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi