November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge kiswaga aunga mkono juhudi za serikali kuboresha mazingira ya elimu

Mkuu wa kitengo cha utamaduni, sanaa na michezo wa Wilaya ya Magu Ndugu Peter Mjaya ( kulia) akimwakilisha afisa elimu msingi akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Salama Ndg. Eliah Kichoge vifaa vya kuezekea nyumba ya walimu vyenye thamani ya shilingi milioni mbili na elfu ishirini vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo la Magu Mhe.Boniventura Destery Kiswaga kwaajili ya kuboresha mazingira ya nyumba za walimu.
Mkuu wa kitengo cha utamaduni, sanaa na michezo Peter Mjaya ( Aliyenyoosha mkono )akifafanua jambo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Magu mara baada ya kutembelea nyumba ya walimu wa Shule ya Msingi Salama baada ya kupkea vifaa vya kuezekea nyumba hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni mbili na elfu ishirini .
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Salama Ndg. Eliah Kichoge (Aliyenyoosha kidole) akitoa Maelezo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu uliombatana na Katibu wa Mbunge wa jimbo la Magu kuhusu nyumba ya walimu yenye uwezo wa kuchukua walimu wawili na familia zao mara baada ya kupokea vifaa vya kuezekea nyumba ya walimu katika hafla ya makibidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi Salama iliyopo Kata ya Ng’haya Halmashauri ya Wilaya ya Magu.
Picha ya pamoja baada ya kupokea vifaa vya kuezekea nyumba ya walimu vyenye thamani ya shilingi milioni nne na elfu ishirini vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo la Magu Mh Boniventura Destery Kiswaga

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha mazingira ya elimu mbunge wa jimbo la Magu mkoani Mwanza Mhe.Boniventura Destery Kiswaga ametekeleza ahadi yake ya kuboresha mazingira ya nyumba za walimu wa shule ya msingi Salama iliypo kata ya Ng’haya Halmashauri ya Magu ambao walikua wanakabiliwa na changamoto ya nyumba ya kuishi kwa walimu.

Katika kutekeleza ahadi hiyo ambayo aliitoa tarehe 14.07.2023 wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ng’haya Mbunge Kiswaga amekabidhi vifaa vya kupaua nyumba ya walimu yenye uwezo wa kukaa walimu wawili na familia zao vyenye thamani ya shilingi Milioni nne na elfu ishirini ambazo amezitoa katika vyanvyo vya mapato binafsi .

Vifaa hivyo ni pamoja na mabati, mbao , waya na misumari ambavyo vitasaidia kuezeka nyumba ya walimu ambayo itatatua changamoto ya nyumba ya kuishi kwa walimu wa shule hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge baada ya kukabidhi vifaa hivyo Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Magu Jonas Masuka amesema kuwa walimu wanafanya kazi kubwa ya kujenga taifa hivyo ni vyema wakaishi katika mazingira salama ili kuboresha utendaji kazi wao wa kuandaa vijana ambao watakua na msaada kwa Taifa.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Afisa mipango wa Halmashauri hiyo Emilian Makomelelo amemshukuru mbunge Kiswaga kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo na kufuatilia kughuli za maendeleo katika jimbo lake.

Makomelelo ameahidi kuwa msaada huo wa vifaa vilivyotolewa vinafanya kazi iliyikusudiwa ya kupaua na kukamilisha nyumba ya walimu kutatua changamoto ya makazi ya walimu ili kuboresha utendaji kazi na hatimaye kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Akizungumza kwa niaba ya Afisa elimu msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu ambaye ni mkuu wa kitengo cha utamaduni, sanaa na michezo Peter Mjaya amesema kukamilika kwa nyumba hiyo kutasaidia walimu kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kuboresha mazingira ya elimu nchini.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Salama Ndg. Eliah Kichoge Maisa ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na kubainisha kuwa vifaa hivyo vitatunzwa ili vitumike kama ilivyokusudiwa .

Naye Mwenyekiti wa CCM kata ya Ng’haya Njile Ngunila Busiya ameishukuru Mbunge Kiswaga kwa kutoa msaada huo huku akibainisha kuwa walimu waikaa katika mazingira mazuri na wanafunzi wanafundishwa katika mazingira bora