Na Mwandishi wetu,Dodoma
WAKULIMA wa mazao mbalimbali hapa nchini, wameishauri Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA),kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ili kuwasaidia kufanya kilimo chenye tija.
Hayo yamebanishwa na Mkulima Joseph Nyimbo wakati akipata maelekezo ya namna ya kujisajili ili aweze kupata mbolea ya ruzuku kutoka serikalini.
“Wakulima wengi hatujui matumizi ya mbolea, tunaishkuru TFRA kwa kuendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa matumizi ya mbolea,”Amesema Nyimbo.
Kwa upande wake Meneja wa TFRA Kanda ya Kati Joshua Ng’ondya amewataka wakulima kutoka kwenye Kilimo cha mazoea na badala yake wafanye kilimo chenye tija ili kujiinua kiuchumi.
Amesema wanapaswa kutumia mbolea sahihi ambazo zinaubora uliothibitishwa na TFRA ili kuendesha kilimo chenye tija ambacho kitawainua kiuchumi.
“Ni vizuri mkazingatia elimu mnayopewa na watalam wa kilimo,ikiwemo kutumia mbolea ya ruzuku kwa ajili ya kustawisha mazao shambani,”Amesema Ng’ondya
Naye Afisa Udhibiti Ubora wa TFRA Steven Gossi amewataka wakulima kujitokeza kujisajili ili waweze kupata mbolea ya ruzuku kutoka serikalini.
Amesema hivi sasa mfumo wa utoaji mbolea umeboreshwa.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja