Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
SERIKALI imewataka mafundi rangi na ujenzi mkoa wa Dar es Salaam, kujiwekeza kwenye mifuko ya akiba ili waweze kujiinua kiuchumi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Chama cha mafundi rangi na ujenzi mkoa huo (UWAMARAUDAR), Afisa Mtendaji Kata ya Buguruni, Ulindula Mtemi amesema mafundi wanajenga majengo yenye thamani isipokuwa uchumi wao hauridhishi.
“Mafundi wanafanya kazi kubwa lakini ukifuatilia kiundani maisha yao, wengi wao hawapo vizuri kiuchumi, kwa upande wetu tutahakikisha tunawapatia mafunzo ya muda mfupi kupitia vyuo vya veta ili wafanye kazi yenye ubora zaidi,” amesema Mtemi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho, Juma Chakusaga amesema wamekuwa wakifanya kazi kubwa lakini maisha yao hayaendani na kazi wanazozifanya, hivyo amewataka baadhi ya kuachana na tabia ya kukaa makundi makundi ili wafike mbali.
“Tunaomba Wizara ya ujenzi isikilize vilio na changamoto zinazotukabili, tunafanya kazi nyingi lakini tunaishi maisha magumu, tunaomba Serikali itutambue ili tuepuke dhana ya kufanya kazi bila kuaminika,” amesema Chakusaga.
Amesema, wapo kwenye mchakato wa kukitangaza chama hicho nchi nzima ili waweze kupata idadi kubwa ya wanachama, ambapo kwa sasa wapo wanachama 140.
Wakati huo huo Diwani wa Kata ya Mnyamani, Shukuru Dege amesema watasaidia kutoa fursa za ajira kwa vijana hao kupitia miradi yao kwa lengo la kuwatoa walipo na kuwapeleka mbali zaidi.
Naye Katibu Mwenezi, John Muhali alisema asilimia kubwa wamekuwa wakiishi maisha magumu licha ya kuwa na kazi ambayo inainua uchumi wa nchi.
Ameongeza kuwa, kumekuwa na tabia ya ukatili wa kijinsia wanaofanyiwa mafundi wanawake na wahusika wa majengo wanayoyajenga jambo ambalo linazalilisha mafundi hao.
“Ninakemea tabia ya kikatili wanaofanyiwa dada zetu wanapokuwa kwenye majukumu yao hali inayochangia kuwadidimiza na kushindwa kutimiza malengo yao, ninaiomba serikali itusaidie,” amesema Mihali.
Chama hicho kilisajiliwa mwaka 2017 chini ya Wizara ya mambo ya ndani.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi