Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu Lissu, amewatusi marais wastaafu, hayati Benjami William Mkapa na mwenzake Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwaita ni wezi walioshiriki kuiba mali za umma katika utawala wao.
Akizungumza katika Mkutano wao uliofanyika Bukoba, mkoani Kagera, Lissu alisema enzi za utawala wao kulifanyika matukio ya wizi na wao wakiwa ni marais wa nchi hii.Alisema jambo hilo linapaswa kukosolewa bila kujali imani zao na mchango wao katika Taifa letu.
“Tuyazungumze haya majimboni kwetu na tujipange kulinda vya kwetu, kwa sababu mimi nilimsema Rais Mkapa kwa wizi wake na akanikamata na kukaa na kesi miaka sita ingawa Mkapa alikuwa mkatoliki kama mimi lakini yeye alikuwa mwizi japo alitembea na limsalaba lake.”
“Sio Mkapa tu, hata huyu naye ni wale wale wezi walioibia nchi yetu na Tegeta Escrow bila kusahau maujambazi mengine aliyofanya katika kipindi cha utawala wake na maujambazi mengine ambapo nilipomsema alinifungulia kesi tatu,”Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti Chadema.
Katika mkutano huo uliofanyika Bukoba, Lissu alitumia muda mwingi kuwatusi viongozi wastaafu akiwamo Hayati Mkapa.
Hata hivyo katika Mkutano huo, Chama hiki kinachojulikana kama Chama Kikuu cha Upinzani, kinaonekana kukosa uungwaji mkono kutokana na mikutano yao kukosa wahudhuriaji wengi kama ilivyotokea kwenye Mkutano wa Temeke, uliofanyika hivi karibuni, jijini Dar es Salaam.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â