Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amekutana na kufanya mazungumzo na mwakilishi wa La Liga nchini Tanzania, Jorge Gazapo kwa ajili ya kuangalia maeneo mbalimbali wanayoweza kushirikiana na wizara katika kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini.
Mwinjuma amekutana na mwakilishi huyo leo Julai 27 2023 jijini Dar es salaam ambapo katika mazungumzo hayo, wamekubaliana kuendeleza soka la vijana kwa La Liga kuweka makambi kila mwaka kwa watoto wenye umri wa miaka 10 mpaka 18 na makocha 50.
Pamoja na hayo wamekubaliana La Liga kuaandaa mafunzo ya ujuzi kwa watoto ambayo yatafanyikiwa ESC Laliga nchini Spain, aidha watoto wenye vipaji watachaguliwa kwa makundi ya chini ya miaka 14 na wengine chini ya miaka 17 na watasafirishwa kwenda Spain kwa ajili ya mafunzo zaidi.
Mwinjuma amemuahidi Mwakilishi wa La Liga nchini Tanzania kumpa ushirikiano wote utakaohitajika ili kufanikisha azma hiyo.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda