Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametoa Rai Kwa washiriki wa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kujadili namna Bora ya kuwezesha rasilimali watu hasa vijana ili kuchochea naendelea.
Hayo ameyasema Leo wakati akifungua kikao Cha kiufundi kilichowakutanisha mawaziri mbalimbali kutoka nchi za Afrika chenye lengo la kujadili mtaji wa rasilimali watu amesema nchi zinapaswa kutafuta namna Bora ya kuboresha nguvu kazi ya vijani Kwani ni kichocheo Cha ukuaji wa uchumi.
Amesema mafanikio na maendeleo ya nchi yanategemewa kutokana na rasilimali watu ambapo uwekezaji katika elimu na miundombinu itasaidia ukuaji wa sekta hiyo.
“Nitoe Rai yangu kwenu kikao hiki Cha kiufundi nilichokifungua kikae kijadiliana namna ya kupata rasilimali Fedha ili kuweza kuendeleza rasilimali watu Kwa kuhakikisha elimu inapatika,Afya na miundombinu yote wezeshi itakayosaidia kukuza na kulea rasilimali watu”amesema Mpango
Aidha mpango amesema serikali ya Tanzania imepiga hatua mbalimbali katika kuhakikisha inalinda na kukuza rasilimali watu Kwa kuhakikisha inatoa elimu Bure Kwa shule za msingi mpaka sekondari lakini pia kuwekeza kwenye makundi maalumu
Ameongeza kuwa Sambamba na kuboresha elimu pia wameweza kuwarudisha shule wasichana waliopata ujauzito shule baada ya kujifungua huku serikali ikiwa na lengo la kupitia sera ya elimu upya ili kutunga Sheria itakayosaidia wanafunza kujifunza kutokana na soko.
“Serikali yà Tanzania tumepiga hatua kubwa kwenye kuhakikisha tunalinda hizi rasilimali watu pamoja na kufanya elimu imfikie Kila mtu lakini pia kwenye sekta ya Afya tumeboresha sana ikiwemo kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.”ameongeza Mpango
Amesema serikali pia imewesesha huduma Kwa kaya masikini lakini pia upatikanaji wa huduma muhimu Kila sehemu
Kwa upande wake Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa kuwekeza kwenye rasilimali watu ni kuchochea maendeleo Kwa taifa hivyo serikali itaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo elimu na afya ili kuhakikisha rasilimali iliyopo inatunzwa.
Amesema mwaka 2017 serikali ilitambulisha sera ya elimu Bure kwa Kwa shule za msingi na sekondari Hali iliyochochea ongezeko la asilimia 80 la wanafunza waliojiandisha shule.
“Tanzania tumepiga hatua mbalimbali ili kulinda rasilimali watu katika sekta ya afya tumeweza kutoa mafunzo mbalimbali pamoja nakuajili watu wenye ujuzi lakini huduma za hospital zimeongeza zaidi ya zahanati 200 zimejengwa na vituo vya Afya 700″amesema Dtk Nchemba
Nae Naibu Waziri Mkuu kutoka nchi ya Capevede Dtk. Olovo Correla amesema ili kutatua changamoto na rasilimali watu nchi za Afrika zinapaswa kujadili namna ya kupunguza umaskini kwenye nchi zao.
Amesema vijana wengi wanakimbia nchi za afrika kutokana na kukosekana kwa fursa kwenye nchi zao.
“Bara Lina watu wengi hasa vijana lakini kumekuwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na elimu,Afya ,ajira na miundombinu ili kuendeleza rasilimali watu lazima tubadilike”amesema Dkt Correla
Ameongeza kuwa waafrika wanapaswa kuishi Kwa utu Kwani bara Lina Kila kitu hivyo washikamane kuondoa umaskini Afrika na kuboresha rasilimali watu
Mkutano wa rasilimali watu umewakutanisha wakuu wa nchi kutoka katika nchi zote za afrika ambao umefanyika katika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam umefunguliwa Leo Kwa kuanza na kikao cha kiufundi kilichowakutanisha mawaziri na kinatarajiwa kukamilika kesho Kwa mkutano wa wakuu wa nchi na kuja na azimio la Dar es salaam.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa