November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakuu wa nchi Afrika kukutana Dar Julai 25,2023,Chalamila awataka wananchi kuchangamkia fursa

Na David John,TimesmajiraOnline.

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam amewataka wananchi wa Mkoa wa huo kuchangamkia fursa za mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaohusu mtaji wa rasilimali watu, kukuza mapato yao na uchumi inayotarajia kufanyika hapa nchini kuazia Julai 25 mwaka huu.

Amesema mkutano huo unatarajia kuwa na watu 1200 kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika na utakuwa na manufaa makubwa katika nchini yetu na hizo ni juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kutokana na utulivu na amani iliyopo hapa nchini.

Chalamila ameyasema hayo Julai 21 mwaka huu jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo na kwa namna mkoa huo ulivyojipanga kupokea wageni mbalimbali wanaotarajia kuhudhuria na wengine wameshafika.

Pia ametoa rai Kwa wakazi wa jiji hilo kuonyesha bashasha na taswira nzuri katika kuwahudumia wageni watakaoshiriki mkutano huo utakaoaza Julai 25 na 26, mwaka huu, Dar es Salaam, kwani utakuwa na manufaa makubwa na utaacha dola zitakazosaidia kukuza uchumi wa nchini.

Aidha amesisitiza kuwa ugeni huo unamanufaa makubwa kwa Watanzania kwani utachangia kukuza uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja.

“Tutakuwa na wageni karibu 1200 ambao watalala katika hoteli zaidi ya 40 hivyo watachangia kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja kupitia sekta ya utalii husasani wa mikutano,”amesema.

Mkuu wa mkoa Chalamila pia ametoa sababu za Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni pamoja na amani utulivu uliopo huku akiwataka wajasiriamali nao kuchangamkia fursa hiyo na kwamba tayari mabanda 100 yatakuwepo katika viwanja hivyo vya mkutano .